Ilani ya Faragha ya Tools for Humanity
- “Data za Programu ya World” inamaanisha data zote za kibinafsi zilizokusanywa na kuchakatwa kupitia matumizi yako ya programu ya World App, kama ilivyobainishwa zaidi katika Sehemu ya 5 hapa chini, isipokuwa data zozote za kibinafsi zinazohusiana na matumizi yako ya mfumo wa Worldcoin au sarafu za Worldcoin (kama vile anwani yako ya pochi na data za miamala, ambazo hatukusanyi).
- Data za Kuthibitisha Stakabadhi inamaanisha data zinazochakatwa unapothibitisha maelezo ili kuyaongeza kwenye World ID yako ya umiliki wa kibinafsi. Hii inamaanisha K.m., kusoma kifaa cha NFC kwenye pasipoti yako ili kuhifadhi maelezo tako ya pasipoti kwenye kifaa chako. Data hizi ziko chini ya udhibiti wako na baada ya kuythibitisha uhalali wa stakabadhi yako, TFH inahifadhi kipande bila utambulisho cha kiwango cha hash cha sahihi ya kipekee ya kriptografia ya maelezo yako (k.m., pasipoti) ili kuhakikisha kwamba kila stakabadhi inaweza kuongezwa mara moja tu kwenye World ID.
- “Data za biashara” inamaanisha data zote za kibinafsi zilizokusanywa na kuchakatwa kupitia njia nyingine za kampuni yetu wakati wa kuwasiliana au njia yoyote nyingine ya kushirikiana au kutangamana nasi kupitia barua pepe, mikutano kwa video au tovuti zetu. Kwa uchakataji data katika muktadha wa Programu ya Orb tafadhali rejelea Ilani ya Faragha ya Programu ya Orb iliyounganishwa kwenye Programu ya Orb. Kwa uchakataji data katika muktadha wa ukusanyaji na majaribio ya data maalum tafadhali rejelea Ilani husika ya Faragha ya Ukusanyaji na Majaribio iliyounganishwa kwenye programu yako ya majaribio. Kwa uchakataji data katika muktadha wa tovuti yetu tafadhali rejelea Sera ya Kuki kwenye tovuti yetu.
- Jitihadi zetu za kulinda faragha yako na data zako
- Maelezo tunayokusanya na kwa nini
- Jinsi tunavyotumia data tunazokusanya
- Mahali ambako tunachakata data zako
- Wakati ambao tunashiriki data zako
- Jinsi data zako zinavyorekodiwa kwenye blockchain ya umma
- Jinsi tunavyotumia kuki
- Muda tunaohifadhi data zako
- Jinsi Ilani hii ya Faragha ilivyo tofauti kwa watoto na vijana
- Haki za kisheria ulizo nazo
- Jinsi ya kuwasiliana nasi kuhusu Ilani hii ya Faragha
- Nambari ya simu.Unaweza kuchagua kuweka nambari yako ya simu ili kuihusisha na akaunti yako. Kwa kibali chako, watumiaji wengine wanaweza kutafuta akaunti yako kwa kutumia nambari yako ya simu. Huenda tukahitaji nambari yako ya simu unapowasilisha ombi la data za mhusika. Misingi ya kisheria ya kuchakata data hizi ni utekelezaji Huduma chini ya Sheria za Mtumiaji.
- Jina la Mtumiaji.Unaweza kuunganisha jina la mtumiaji kwenye anwani ya pochi lako na kubadilisha jina la mtumiaji wakati wowote.
- Tarehe ya Kuzaliwa.Unaweza kufichua tarehe yako ya kuzaliwa ili kuhakikisha uambatanaji na vigezo vya umri unaohitajika. Hatutawahi kuhifadhi tarehe yako ya kuzaliwa lakini ni “checksum” ya data hizo na kama una umri wa zaidi ya miaka 18 au la.
- Maoni na mawasiliano kutoka kwako.Hii inajumuisha barua pepe zozote, ujumbe wowote, au mawasiliano mengine yoyote unayotutumia kupitia barua pepe au tovuti za mitandao ya kijamii ya wahusika wengine. Hii inaweza kujumuisha kuchakata anwani za barua pepe au wasifu za mitandao ya kijamii ikiwa unataka kuwasiliana nasi kupitia mbinu kama hizo. Tunaweza kutumia mtoa husuma mwingine ili kuwezesha utafiti kuhusu matumizi yako ya Huduma zetu. Misingi ya kisheria ya kuchakata data hizi ni utekelezaji Huduma chini ya Sheria za Mtumiaji.
- Waasiliani kwenye kitabu cha waasiliani.Unaweza kuruhusu Programu kufikia kitabu chako cha anwani ili kuwezesha kipengele ambacho kinakurahisishia kutafuta na kutangamana na watumiaji wengine ambao huenda wakawa katika kitabu chako cha anwani. Misingi ya kisheria wa kuchakata data hizi ni nia halali ya mhusika kupatikana ndani ya Programu na nia ya mtumiaji aneyeshiriki kupata waasiliani wake ndani ya Programu.
- Maelezo ya Eneo. Unaweza kuamua kuwezesha huduma inayotegemea eneo (kama vile kipengele kinachokuruhusu kumpata Mhudumu wa Orb aliyekaribu nawe). Ni kwa idhini yako maalum pekee, tunaweza kukusanya maelezo kuhusu eneo lako kupitia GPS ili kuwezesha husuma inayotegemea eneo ili kukuonyesha kifaa cha Orb kilicho karibu nawe. Unaweza kubadilisha vibali vyako wakati wowote katika mipangilio ya kifaa chako. Ikiwa hayuko nchini Korea Kusini tunaweza pia kuhifadhi kadirio la eneo lako bila kuhusishwa na akaunti yako ya Programu ya World. Tunatumia data hizi ili kuboresha huduma zetu haswa lakini sio tu katika kuchagua maeneo ya kifaa cha Orb.
- Soko la P2P. Ikiwa unatumia Huduma za Soko la P2P (zinakopatikana) ambazo zinakuwezesha kununua sarafu za kidijitali kutoka kwa watumiaji wengine, basi tunaweza kuchukua maelezo ya ziada kama vile anwani yako ya pochi, maelezo yako ya mawasiliano, na nambari ya akaunti yako inayohusishwa na muamala (kama vile nambari yako ya M-PESA). Tunarekodi data za muamala kama sehemu ya kutoa Huduma za Soko la P2P. Pia tunaweza kuchukua maelezo ya ziada ili kuambatana na mahitaji husika ya KYC.
- Metadata za kifaa.Ikiwa unatumia Programu tunakusanya metadata kutika kwenye kifaa chako ili kuhakikisha kwamba Programu inafanya kazi vizuri na kwamba haukiuki Sheria na Masharti yetu. Hii inajumuisha kukusanya vitambulishi vya kifaa na anwani za IP.
- Data za World ID za Kifaa.Pia tunachakata metadata za kifaa chako ili kutathmini utambulisho wa kipekee wa kifaa. Msimbo wa utambulisho huu unatumika kama ishara inayothibitisha ubinafsi wako unapotumia World ID ya kifaa.
- Jina la kwanza na la mwisho.Tunaweza kuchakata jina lako la kwanza na la mwisho ili kutimiza nia halali ya kudumisha na kudhibiti uhusiano wa kibiashara pamoja nawe.
- Anwani ya Barua Pepe.Pia unaweza kupatiana anwani yako ya barua pepe kwenye orodha yetu ya mapasho ili kufahamishwa kuhusu habari mpya za mradi wa Worldcoin. Huenda tukahitaji anwani yako ya barua pepe unapowasilisha ombi la mmiliki data. Tunaweza kuchakata anwani yako ya barua pepe ili kutimiza nia halali ya kudumisha na kudhibiti uhusiano wa kibiashara pamoja nawe.
- Nambari ya Simu.Tunaweza kuchakata nambari yako ya simu ili kutimiza nia halali ya kudumisha na kudhibiti uhusiano wa kibiashara pamoja nawe.
- Data za Biashara. Ikiwa una uhusiano wa kibiashara nasi (kama vile wewe ni Mhudumu wa Orb au mletaji wetu), basi tunaweza kuhitaji maelezo kama vile majina, anwani ya barua, barua pepe, nambari ya simu, anwani ya pochi, na nyaraka zingine (kama vile kitambulisho chako cha serikali) kama sehemu ya kuimarisha uhusiano huo wa kibiashara na ili kutimiza majukumu ya kumjua-mteja-wako. Tunaweza kutumia huduma za wahusika wengine, kama vile Onfido, ili kutusaidia kukusanya na kuhakiki maelezo na nyaraka zilizotajwa hapa juu ili kutimiza majukumu ya kumjua-mteja-wako.
- Data za utumaji ombi. Ikiwa ungependa kufanya kazi nasi ni lazima ututumie ombi lako linalojumuisha barua ya kujieleza pamoja na CV na vile vile maelezo ya kibinafsi ambayo ungependa kufichua.
- Data za Blockchain. Tunaweza kuchambua data za blockchain ya umma ili kuhakikisha kwamba watu wanaotumia Huduma zetu hawajihusishi katika shughuli haramu au zilizopigwa marufuku chini ya Sheria za Mtumiaji, na ili kuchambua mitindo ya miamala kwa madhumuni ya utafiti na utengenezaji.
- Huduma za Uthibitishaji Utambulisho. Tunaweza kupata maelezo kutoka kwa huduma za wahusika wengine kwa kutumia data zako ili kuthibitisha utambulisho wako ikiwa inahitajika na sheria (kama vile mahitaji husika ya kumjua-mteja-wako). Ili kufafanua,hatutumiidata zako za bayometriki tunapothibitisha utambulisho wako kama inavyohitajika na sheria.
- Hifadhidata za talanta. Huenda tukakusanya data kutoka kwa vyanzo mbali mbali ili kupeana kazi kwa watu walio na talanta.
- Vitambulishi vya Mtandaoni:Maelezo ya eneo la kijiografia (tazama hapa juu), mfumo msingi wa uendeshaji kompyuta au simu tamba, jina na toleo la kivinjari, na anwani za IP. Katika matukio chache sana data hizi pia zinawekwa katika rekodi yetu ya ugunduaji ulaghai na mtiririko haramu wa fedha. Pia vinahudumu kama njia ya kutoa huduma iliyostawi na bila ulaghai ya maunzitepe yetu.
- Data za Matumizi:Data za uthibitishaji, maswali ya kiusalama, na data nyingine zilizokusanywa kupitia kuki na teknolojia sawa.
- Kuki: faili ndogo za data zinazohifadhiwa kwenye hifadhi yako au kwenye kumbukumbu ya kifaa chako zinazotusaidia kuimarisha Huduma zetu na hisia zako, kuona ni maeneo na vipengele gani vya Huduma zetu ni maarufu, na kuhesabu mara unayotembelea Huduma. Ili kupata misingi ya kisheria ya kuchakata data hizo tafadhali rejelea Sera yetu ya Kukiambapo tumeelezea aina tofauti ya kuki tunazotumia.
- Data za miamala
- Data za ubonyezaji maeneo ya skrini
- Metriki za utendakazi
- Vigunduaji ulaghai (ingawa data za kibinafsi zinatumika kwa malengo haya, pia)
- Kutoa na kudumisha bidhaa na huduma zetu chini ya Sheria za Mtumiaji. Huduma hizi zinajumuisha:
- Programu ambapo watumiaji wanaweza kudhibiti World ID yao na sarafu zake za kidijitali na pia kujifunza kuhusu sarafu za kidijitali kwa ujumla na mradi wa Worldcoin haswa;
- Programu ya Mhudumu ambapo Wahudumu wa Orb wanaweza kudhibiti na kusimamia vifaa vyao vya Orb na takwimu za vifaa hivyo;
- Soko la P2P ambapo tunapatanisha watumiaji na maajenti (haihusu watumiaji walio nchini Ujerumani au wana makazi yao au ofisi rasmi nchini Ujerumani);
- Kuimarisha na kutengeneza bidhaa na huduma zetu, ikijumuisha kuondoa hitilafu na kukarabati kasoro kwenye Huduma zetu.
- Kufanya utafiti wa sayansi ya data.
- Kuchambua matumizi yako ya Huduma zetu ili kukupa usaidizi bora.
- Kukuwezesha kuchapisha maelezo kwenye blockchain ili kuthibitisha wewe ni mtu binafsi.
- Kutumia anwani ya pochi lako ili kukutumia sarafu za kidijitali ambazo tunahusika nazo.
- Kuambatana na sheria husika kama vile sheria na vikwazo vya dhidi ya utakatishaji pesa. Hii inajumuisha:
- Kutumia anwani yako ya IP ili kuwazuia watu binafsi kutoka mataifa au nchi zilizopigwa marufuku kutumia Huduma;
- Kujibu maombi ya mmiliki data chini ya sheria husika za ulindaji data kama vile maombi ya kufikia au kufuta data;
- Kufuatilia mitiririko ya fedha ambazo zinaweza kuwa chafu k.m. anwani zilizowekwa kwenye orodha nyeusi; na
- Kuambatana na sheria husika kama vile kanuni dhidi ya maudhui haramu.
- Kushughulikia maombi ya huduma, malalamishi na maswali yako kama mteja.
- Kusuluhisha migogoro, kutatua masuala, na kutekeleza makubaliano yetu nawe, pamoja na Ilani hii ya Faragha na Sheria za Mtumiaji.
- Kuwasiliana nawe kuhusiana na visasisho kwenye Huduma.
- Tunakagua uhalali wa stakabadhi yako (kama ni pasipoti hii inafanywa kupitia thibitisho la nchi yako).
- Tunakuthibitisha kama mmiliki halali wa stakabadhi hiyo (kwa pasipoti hii inafanywa kwenye kifaa chako kupitia picha ya uso wako (selfie) ambayo haihifadhiwi kamwe).
- Tunasimba, kuweka sahihi na kuhifadhi data za stakabadhi yako katika mazingira salama kwenye kifaa chako.
- Hatuwezi kufikia maelezo ya kibinafsi yaliyo kwenye stakabadhi yako.
- Kisha baadaye unaweza kusambaza maelezo haya na wahusika wanaohitaji kupitia ulinzi wa teknolojia ya World ID (k.m., unaweza kuthibitisha kwamba una umri wa anaglau miaka 18 bila kuvumbua umri wako haswa au wewe ni nani).
- Kwa pasipoti, TFH inadumisha tu maelezo bila utambulisho wa kiwango cha hash cha sahihi ya kipekee ya kriptografia ya pasipoti yako ili kuhakikisha kwamba kila pasipoti inaweza kuthibitishwa mara moja tu.
- Tunapofanya kadri tuwezayo ili kuhakikisha kwamba wanakandarasi wetu wadogo wana jukumu la kimkataba la kulinda data zako vya kutosha, wanakandarasi hawa wadogo huenda wasiwe chini ya sheria za faragha ya data za nchi yako. Wakandarasi wakichakata data zako kwa njia isiyo ya kisheria bila idhini, basi huenda ikawa vigumu kudai haki zako za faragha dhidi ya wakandarasi hao. Tunazuia hatari hii kwa kuwa na makubaliano dhabiti ya uchakataji data na wakandarasi wetu ambayo inawabidi kulinda data kwa kiwango cha GDPR na kutimiza maombi ya mhusika.
- Kuna uwezekano kwamba sheria ya faragha ya data nchini mwako haiendanishi na sheria za faragha ya data nchini Marekani, au katika EU. Daima tutajaribu kuambatana na kiwango cha juu zaidi cha ulindaji data ambacho tunatumia.
- Kuna uwezekano kwamba data zako zitaweza kufikia na maafisa au mamlaka za kiserikali. Katika matukio hayo tumejitayarisha kupinga mahakamani ombi lolote la kiserikali la kufikia data ambalo si halali, linapita mipaka, au si la kisheria. Aidha tunatumia usimbaji wa hali ya juu ili kuzuia ufikiaji bila idhini.
- Tunazishiriki kwa njia salama;
- Kuchukua hatua kuhakikisha kwamba inashughulikiwa kwa njia ambayo inaendanisha na jitihada zetu kwa faragha yako; na
- Tunazuia kampuni zingine kutozitumia kwa malengo yao binafsi.
- Tunazambazia Asasi ya Worldcoin:Tunaweza kutenda kama wachakataji wa Asasi ya Worldcoin wa data za kibinafsi kwa niaba ya Worldcoin (tafadhali tazama kauli ya faragha ya Worldcoin ili kupata maelezo zaidi).
- Kusambaza ndani ya shirika letu:Tunafichua tu data kwa wanatimu wetu ambao wanahitaji kuzifikia ili kuweza kufanya kazi na majukumu yao. Tunafichua tu kiwango cha data ambacho kinahitajika ili kufanya kazi na majukumu fulani na kuwa na mfumo ulio na udhibiti mkali wa ufikiaji.
- Kusambaza kwa wachuuzi na watoa huduma nje ya shirika letu:Tunafichua tu data kwa watoa huduma ambao huduma zao tunazitegemea ili kuchakata data na kukupa Huduma zetu. Tunafichua tu data kwa wachuuzi wa huduma ya uthibitishaji utambulisho ikiwa inahitajika na Sheria (yaani, mahitaji-ya-kumjua-mteja-wako).
- Kategoria za watoa huduma hao ni:
- Watoa huduma ya wingu (aina zote za data)
- Watoa bidhaa za SaaS; tunatumia bidhaa za SaaS katika kategoria zifuatazo:
- Menejimenti ya hifadhidata na miundombinu
- Usalama wa Data
- Uteuzi
- Mawasiliano
- Utafiti
- KYC/KYB yaani. kukagua hati rasmi
- Menejimenti ya maombi ya data
- Usaidizi wa kiufundi
- Huduma kwa watumiaji
- Wataalamu wa nje
- Watengenezaji maunzitepe maalum
- Wataalamu wa kisheria
- Washauri wa ushuru
- Benki
- Watoa huduma ya kuweka lebo (chini ya ulinzi maalum pekee)
- Huduma za ukaguaji historia za watumaji maombi na Wahudumu wa Orb
- Kwa watekelezaji sheria, maafisa, au wahusika wengine:Tunaweza kufichua data zako ili kuambatana na sheria husika na kutii mahitaji ya lazima ya kisheria. Kwa uangalifu tunazingatia kila ombi ili kubaini kana kwamba ombi hilo linaambatana na sheria na, panapofaa, tunaweza kupinga maombi ambayo si halali, yanayopita mpaka, au yasiyo ya kisheria. Tunaweza kushiriki data za kibinafsi na polisi na mamlaka nyingine za serikali ambapo tunaamini ni muhimu ili kuambatana na sheria, kanuni au mchakato au jukumu nyingine la kisheria.
- Tunaweza kushiriki maelezo yako ya kibinafsi ikiwa tunaamini kwamba matendo yako hayaendanishi na Sheria zetu za Mtumiaji, ikiwa tunaamini kwamba umekiuka sheria, au ikiwa tunaamini kwamba ni muhimu ili kulinda haki zetu, mali yetu, na usalama wetu, watumiaji wetu, umma, na wengine.
- Tunaweza kushiriki maelezo yako ya kibinafsi na mawakili wetu na washauri wengine wataalamu ambapo ni muhimu ili kupata ushauri au vinginevyo kulinda na kudhibiti bia zetu za kibiashara.
- Tunaweza kushiriki maelezo yako ya kibinafsi kuhusiana, au wakati wa majadiliano kuhusiana na, ununuzi wowote, mali ya kampuni kuuzwa, ufadhili, au sehemu ya biashara au biashara yote kununuliwa na kampuni nyingine.
- Data, ikijumuisha maelezo yako ya kibinafsi, zinaweza kushirikiwa miongoni mwa kampuni mzazi, washirika, na kampuni tanzu za siku zijazo na kampuni nyingine chini ya udhibiti na umiliki wa pamoja.
- Tunaweza kushiriki maelezo yako ya kibinafsi kwa idhini yako au kwa maagizo yako.
- Una haki ya kupata kutoka kwetu wakati wowote baada ya kutuma ombi maelezo kuhusu data za kibinafsi tunazochakata kukuhusu. Una haki ya kupata kutoka kwetu data za kibinafsi zinazokuhusu.
- Una haki ya kuagiza kwamba mara moja tusahihishe data za kibinafsi zinazokuhusu ikiwa si sahihi.
- Una haki ya kuagiza kwamba tufute data za kibinafsi zinazokuhusu. Mahitaji haya yanaonyesha haki ya kufutwa ikiwa data za kibinafsi si muhimu tena kwa madhumuni ambayo ilifanya zikusanywe au kuchakatwa, mradi mahitaji ya kufuta chini ya sheria husika yamebainishwa (k.m. sheria kadhaa za maeneo ya mamlaka zinatuhitaji kuhifadhi maelezo ya miamala kwa kipindi fulani cha muda)
- Una haki ya kuondoa kwa hiari idhini yako ya uchakataji wowote wa data kwa idhini au kukataa uchakataji wa data ikiwa si kwa idhini.
- Una haki ya kupata kutoka kwetu wakati wowote baada ya kutuma ombi maelezo kuhusu data za kibinafsi tunazochakata kuhusiana na ndani ya wigo wa Kifungu cha 15 cha GDPR.
- Una haki ya kuagiza kwamba mara moja tusahihishe data za kibinafsi zinazokuhusu ikiwa si sahihi.
- Una haki, chini ya hali zilizoelezewa katika Kifungu cha 17 cha GDPR, kuagiza kwamba tufute data za kibinafsi zinazokuhusu. Mahitaji haya yanaonyesha haki ya kufutwa ikiwa data za kibinafsi si muhimu tena kwa madhumuni ambao ilifanya zikusanywe au kuchakatwa, na pia katika matukio ya uchakataji usio wa kisheria, uwepo wa pingamizi au uwepo wa jukumu la kufuta chini ya sheria la Umoja au sheria ya Jimbo kwa ambayo tupo chini yake.
- Una haki ya kuagiza kwamba tuwekee vikwazo uchakataji kulingana na Kifungu cha 18 cha GDPR.
- Una haki ya kupokea kutoka kwetu data za kibinafsi zinazokuhusu ambazo umetupatia kwa umbizo sambamba, linalotumika kwa kawaida, na linalosomeka na mashine kulingana na Kifungu cha 20 cha GDPR.
- Wakati wowote, kwa misingi inayohusiana na hali yako haswa, una haki ya kupinga uchakataji wa data za kibinafsi zinazokuhusu ambao umefanywa, na kadhalika, kwa misingi ya Kifungu cha 6 (1) sentensi ya 1, eneo la f kwenye GDPR, kulingana na Kifungu cha 21 cha GDPR.
- Una haki ya kuwasiliana na mamlaka adilifu ya usimamizi endapo kutakuwa na malalamishi kuhusu uchakataji data unaofanywa na mdhibiti. Mamlaka ya usimamizi inayowajibika ni: the Bavarian State Office for Data Protection Supervision (Bayerisches Landesamt für Datenschutz).
- Ikiwa uchakataji wa data za kibinafsi unategemea idhini yako, una haki chini ya Kifungu cha 7 cha GDPR una haki ya kughairi idhini yako ya matumizi ya data zako za kibinafsi wakati wowote katika siku zijazo, ambapo kughairi huku ni rahisi kufanya kama ilivyo kuwa rahisi kupatiana idhini. Tafadhali kumbuka kwamba kughairi kunaathiri tu siki zijazo. Uchakataji uliofanyika kabla ya kughairi hauathiriki.
- Tunapotuma data hadi kwenye nchi ambayo hatuna uamuzi wa utoshelevu, tunatumia EU Standard Contractual Clauses (Vipengee vya Kimkataba vya Kawaida vya EU). Kwa sasa tunatuma tu data za kibinafsi hadi Marekani.
- Ikiwa uchakataji wa data za kibinafsi unategemea idhini yako, una haki chini ya Kifungu cha 7 cha GDPR una haki ya kughairi idhini yako ya matumizi ya data zako za kibinafsi wakati wowote katika siku zijazo, ambapo kughairi huku ni rahisi kufanya kama ilivyo kuwa rahisi kupatiana idhini. Tafadhali kumbuka kwamba kughairi kunaathiri tu siki zijazo. Uchakataji uliofanyika kabla ya kughairi hauathiriki. Tafadhali pia kumbuka kwamba kuchakata hayo hakutegemei idhini na hivyo hakuathiriki na uondoaji idhini.
Jina la Mpokeaji | Malengo ya matumizi ya mpokeaji | Vipengee vya maelezo ya kibinafsi vya kutumwa kwa mpokeaji | Vipindi vya kuhifadhiwa na mpokeaji |
Tools for Humanity GmbH | Malengo yaliyoelezewa katika ilani hii katika sehemu ya 6 hapa juu. | Vipengee vilivyoelezewa katika ilani hii katika sehemu ya 5 hapa juu | Vipindi vya uhifadhi vilivyooelezewa katika ilani hii katika sehemu ya 11 hapa juu. |
NYONGEZA YA G - BRAZILI
G.1 Sheria Husika, Mdhibiti na Opereta
Ikiwa unaishi nchini Brazili, ikiwa data zako za kibinafsi zilizkusanywa nchini Brazili, au ikiwa unatumia Huduma zetu nchini Brazili, sheria husika ni Sheria Na. 13,709/2018 (Sheria Jumla za Ulinzi wa Data, au “LGPD”).
G.2 Haki ya kukataa
Una haki ya kukataa matumizi ya data zako za kibinafsi kwa malengo ambayo hayategemei idhini ikiwa malengo hayo hayaambatani na LGPD. Ukiamua kukataa, hatutatumia tena maelezo yako ya kibinafsi ili kutengeneza na kuboresha vipengele na huduma ya Huduma zetu.
Kumbuka kwamba ukikosa tupatiana au ukikosa kuruhusu ukusanyaji au uchakataji wa data fulani za kibinafsi, inaweza kuathiri ubora wa huduma yako, huenda tukashindwa kutimiza malengo ya Huduma zetu, au huenda tukashindwa kukupa Huduma fulani.
Katika hali zingine, data zako zinaondolewa utambulisho, kumaanisha haziwezi kukutambulisha tena. Hauwezi kukataa matumizi ya data bila utambulishi kwa sababu haziruhusu utambulishwe, kama ilivyobainishwa kwenye LGPD. Tunatumia data hizi bila utambulisho ili kuboresha bidhaa na huduma zetu.
G.3 Haki za kisheria chini ya LGPD
Kulingana na LGPD, una haki ya kuthibitisha uwepo wa uchakataji, ufikiaji, urekebishaji, au ombi la uhamishaji wa data zilizochakatwa. Aidha, unaweza kuomba maelezo ya mashirika ya umma na kibinafsi ambayo kwa pamoja tunatumia data zako za kibinafsi. Pia unaweza kuomba maelezo kuhusiana na uwezekano wa kutopatiana idhini na madhara yake, na uombe kufutwa kwa data zilizochakatwa kwa idhini. Unaweza kuchagua maelezo yako kufutwa kwenye Programu ya World kwenye menyu ya Mipangilio.
Katika hali fulani, una haki ya kukataa au kuweka kipimo cha jinsi tunavyochakata data zako za kibinafsi, au kuondoa idhini yako, ambayo tunategemea ili kuchakata maelezo unayopatiana.
Unaweza kutekeleza haki zako chini ya LGPD kwa kuwasilisha ombi kwa DPO wetu ukitumia maelezo ya mawasiliano yaliyo katika sehemu ya H.4 hapa chini au kupitia lango letu la maombi la mtandaoni. Ukihisi kwamba haki zako hazijazingatiwa vya kutosha, unaweza kuandikisha lalamishi kwa Autoridade Nacional de Proteção de Dados Pessoais (ANPD) kwa kujaza fomu inayopatikana kwenye kiungo hiki: https://www.gov.br/anpd/pt-br/canais_atendimento/cidadao-titular-de-dados.
G.4 Kutuma Data Zako za Kibinafsi Kimataifa
Ikiwa LGPD inatumika kwako, na tumekusanya data zako za kibinafsi, tunaweza pia kuzituma nje ya nchi. Hata hivyo, kila wakati tutahakikisha kwamba data zako za kibinafsi zinatumwa tu hadi nchi za kigeni aukwa mashirika ya kimataifa ambayo yana kiwango cha ulinzi ambacho ni sawa na cha LGPD, kama inavyotambuliwa katika maamuzi ya kutosha uanayotolewa na ANPD. Endapo hakutakuwa na uamuzi kuhusu kutosha, tutaendelea kufuata kiwango cha ulinzi ambacho angalau ni sawa na kinachotolewa na LGPD kwa kutumia Vifungu vya Kimkataba vilivyowekwa katika kanuni za ANPD au tunapopokea idhini yako maalum ya kutuma kimataifa.
Kwa Nini Tunachakata Data | Ni Data Gani za Kibinafsi Zinachakatwa | Msingi wa Kisheria wa Uchakataji | Kipindi cha Kuhifadhi Data |
Kutengeneza akaunti yako katika Programu ya World | Anwani ya pochi, metadata, jina la mtumiaji | Utekelezaji mkataba | Kipindi cha matumizi ya huduma au mpaka uombe data hizo zifutwe. |
Kuhakikisha una umri unaofaa | Tarehe ya kuzaliwa | Jukumu la kisheria | Tarehe yako haswa ya kuzaliwa haihifadhiwi. Tunahifadhi tu kama umefikisha miaka 18. Tunahifadhi maelezo kwa kipindi cha matumizi ya huduma au mpaka uombe data hizo zifutwe. |
Ili kuwezesha waasiliani wako kuwasiliana na kufanya miamala nawe kwa urahisi | Nambari ya simu | Idhini | Kipindi cha matumizi ya huduma au mpaka uombe data hizo zifutwe. |
Ili kukuwezesha kuwasiliana na kufanya miamala na waasiliani wako kwa urahisi | Waasiliani katika kitabu cha waasiliani | Idhini | Kipindi cha matumizi ya huduma au mpaka uombe data hizo zifutwe. |
Ili kukuonyesha vifaa vya Orb vilivyo karibu nawe | Maelezo ya Eneo | Idhini | Hadi miezi 24. |
Ili kuzuia ulaghai katika muktadha wa kuzuia akaunti | Metadata, anwani ya IP address, kitambulisho cha Kifaa | Nia halali, haswa nia ua kuzuia aina fulani ya ulaghai (ORODHA YA AINA) | Hadi miezi 24. |
Ili kuhakikisha huduma zinaruhusiwa katika nchi yako | Anwani ya IP, maelezo ya eneo | Jukumu la kisheria | Hadi miezi 24. |
Ili kuonyesha pochi la umiliki wa kibinafsi na kuonyesha kiolesura cha miamala ya pochi | Anwani ya pochi, data za miamala | Utekelezaji mkataba | Hakuna maelezo ya kibinafsi yanayohifadhiwa katika muktadha huu. |
Ili kuonyesha World ID yako ya umiliki wa kibinafsi na kuonyesha kiolesura cha uthibitishaji | Maelezo ya World ID | Utekelezaji mkataba | Hakuna maelezo ya kibinafsi yanayohifadhiwa katika muktadha huu. |
Ili kuonyesha Stakabadhi zako za umiliki wa kibinafsi na kuonyesha kiolesura cha kushiriki Stakabadhi hizo | Maelezo ya Stakabadhi, maelezo ya uhalali wa stakabadhi | Utekelezaji mkataba | Hakuna maelezo ya kibinafsi yanayohifadhiwa katika muktadha huu. |
Ili kuchambua na kutoa huduma zetu na kuendesha mazoesi ya tafiti za data | Data za matumizi na metadata, data za miamala za hadharani | Idhini | Hadi miezi 24. |
Ili kuambatana na sheria husika kama vile sheria na vikwazo dhidi ya utakatishaji pesa | Data za miamala, anwani ya pochi | Jukumu la kisheria | Kipindi cha matumizi ya huduma. |
Ili kuambatana na sheria husika kama vile kanuni za maudhui | Maudhui ya Miniapp | Jukumu la kisheria | Kipindi cha matumizi ya huduma. |
Ili kuwezesha mawasiliano na uuzaji | Anwani ya barua pepe, arifa za papo hapo | Nia Halali | Hadi miezi 24. |
Mawasiliano kutoka kwako | Nia Halali | Hadi miezi 24. | |
Maoni kutoka kwako | Nia Halali | Hadi miezi 24. | |
Kushughulikia maombi ya huduma, malalamishi na maswali yako kama mteja. | Maelezo ya mawasiliano na barua pepe au jina la wasifu wa mtandao wa kijamii ikiwa unataka kuwasiliana nasi kupitia mbinu kama hizo | Utekelezaji mkataba | |
Ili kuhakikisha programu yako inafanya kazi vizuri | Metadata | Utekelezaji mkataba | Hadi miezi 24. |
Ili kuthibitisha kifaa chako | Data za World ID ya Kifaa (alama ya kidole ya kifaa) | Utekelezaji mkataba | Kipindi cha matumizi ya huduma. |
Kusuluhisha migogoro, kutatua masuala, na kutekeleza makubaliano yetu nawe, pamoja na Ilani hii ya Faragha na Sheria za Mtumiaji. | Kipindi cha matumizi ya huduma. |
Kwa Nini Tunachakata Data | Ni Data Gani za Kibinafsi Zinachakatwa | Msingi wa Kisheria wa Uchakataji | Kipindi cha Kuhifadhi Data |
Mawasiliano | Nambari ya simu, anwani ya barua pepe, Jina | Nia halali, yaani, nia ya kuwasiliana na washirika wa kibiashara. | Kipindi cha uhusiano wa kibiashara au mpaka uombe data hizo zifutwe. |
Kudumisha na kudhibiti uhusiano wa kibiashara | Nambari ya simu, anwani ya barua pepe, Jina, data za kampuni | Nia halali yaani nia ya kudumisha na kudhibiti uhusiano wa kibiashara na washirika wa kibiashara. | Kipindi cha uhusiano wa kibiashara au mpaka uombe data hizo zifutwe. |
Kutimiza majukumu ya KYC | Data za pasipoti, Data za kampuni | Jukumu la kisheria | Kipindi cha uhusiano wa kibiashara na hadi miaka 3 baada ya kusitishwa. |
Ili kuchakata programu yako | Data za programu | Idhini na hatua kwa ombi la mmiliki data kabla ya kuingia kwenye mkataba. | Hadi miezi 3 kama chaguomsingi au muda mrefu zaidi ikiwa unakubali kuwa katika kundi la talanta. |