logo

Kituo cha Sheria

  • Ilani ya Faragha ya Tools for Humanity

  • Sheria na Masharti ya Mtumiaji ya Tools For Humanity

  • Kuki ya Faragha ya Tools for Humanity

  • Law Enforcement Requests

  • Privacy Notice – Research and Development

  • Developer Rewards Terms and Conditions

Sheria na Masharti ya Mtumiaji ya Tools For Humanity

Toleo: 3.37Kuanzia February 14 2025

Sheria na Masharti ya Mtumiaji ya Tools For Humanity

Karibu kwenye Programu ya World! Sheria hizi baina yako na Tools for Humanity Corporation, kampuni ya Delaware ("TFH", au “sisi”) zinatawala matumizi yako na ufikiaji wako wa tovuti na programu zetu, ikijumuisha Programu ya World na Programu ya Operator (kwa pamoja, “Programu”), na utendaji, maudhui, na huduma zote husika tunazokupatia (kwa pamoja, "Huduma" au “Huduma Zetu”) kuhusiana na World Network (“World Network”) na mfumo mzima.

Tafadhali soma Sheria hizi kwa uangalifu kabla ya kutumia na kufikia Huduma. Kwa kufikia na kutumia Huduma zozote tunazotoa, pamoja na idhini yako ya Sheria hizi, moja kwa moja unakubali kuwa chini ya Sheria hizi na chini ya Ilani yetu ya Faragha, ambayo imejumuishwa kama sehemu ya Sheria hizi. Tafadhali kumbuka sehemu hizi muhimu za Sheria hizi:

Unakubali kusuluhisha migogoro yoyote baina yako na TFH kupitia mchakato wa usuluhishaji badala ya mahakamani. Ikiwa unaishi Korea Kusini, badala yake unaweza kuchagua kusuluhisha mgogoro katika mahakama yenye ustadi nchini humo. Tafadhali pitia Sehemu ya 15 hapa chini ili kupata maelezo.

Bidhaa za Crypto, ikijumuisha Sarafu za Kidijitali, hazijawekewa sheria na zinaweza kuwa hatari sana. Kunaweza kosa suluhu ya kisheria kwa hasara zozote zinazotokana na miamala hiyo.

Hakuna kitu chochote katika Huduma kinaashiria ofa ya kuuza, au ushawishi wa ofa ya kununua, hisa au Sarafu zozote za Kidijitali. Huduma hazijumuishi ushauri wa uwekezaji. Kumiliki, kununua, au kuuza Sarafu zozote za Kidijitali (kama ilivyobainishwa katika Sehemu ya 2.1 hapa chini) huenda ikawa haijaruhusiwa mahali unakoishi, na ni wajibu wako kuambatana na sheria zote husika. Tafadhali zingatia kama utanunua, kuuza, kutumia, au kumiliki Sarafu za Kidijitali ni mwafaka kwako katika hali yako ya kifedha na uelewa wako wa Sarafu za Kidijitali. Thamani ya Sarafu za Kidijitali huenda ikabadilika kwa haraka na huenda zikapoteza thamani yake yote.

Aidha, sarafu za WLD (“WLD”) hazikusudiwi kupatikana ili kutumiwa, kununuliwa, au kufikiwa na watu wa Marekani, ikijumuisha raia wa Marekani, wakaazi au watu walio nchini Marekani, au kampuni zilizosajiliwa, zilizoko, au makao yake ni Marekani, au walio na maajenti waliosajiliwa nchini Marekani. Hatufanyi WLD kupatikana kwa watu hao wa Marekani. Zaidi ya hayo, unakubali kwamba hautawauzia, kuwatumia au kuwasaidia watu wa Marekani kupata WLD. Maelezo zaidi kuhusu hatari zinazohusishwa na WLD yanaweza kupatikana hapa.

1. Wigo wa Sheria

1.1 Faragha na Data Zako. Unapotumia Programu, unaweza kutupatia kategoria za maelezo ya kibinafsi, kama vile jina lako au nambari ya simu. Ukitupatia maelezo ya kuthibitisha wewe ni mtu binafsi na udai sarafu zako za WLD, basi unaweza kupatiana kategoria maalum za data nyeti za kibinafsi, kama vile maelezo yako ya bayometriki. Ilani yetu ya Faragha inaelezea data tunazokusanya kutoka kwako na jinsi tuanvyozitumia. Tafadhali usitumie Huduma ikiwa hautaki tukusanye au kutumia data zako kwa njia ambayo imeelezewa katika Ilani ya Faragha.

1.2 Ustahiki. Kurasa za wavuti zinazoelezea huduma zetu zinaweza kufikika kote ulimwenguni, lakini hii haimaanishi kwamba Huduma zote au vipengele vyote vya huduma ni halali au zinapatikana nchini mwako. Hauwezi kutumia zana za VPN au zana sawa na hizo ili kuepuka vikwazo vyovyote. Ni wajibu wako kuhakikisha kwamba matumizi yako ya Huduma zetu ni halali mahali ambako unazitumia. Huduma Zetu hazipatikani kwa lugha zote. Huduma zetu ni halali mahali ambako unazitumia. Huduma Zetu hazipatikani kwa lugha zote. Ili kutumia Huduma, ni lazima uambatane na Sheria hizi pamoja na sheria zote husika. Hauwezi kutumia Huduma Zetu kuendesha, kukuza, au kuwasaidia wengine kufanya shughuli zozote haramu au zisizo za kisheria.

Aidha, ni lazima utimize vigezo vyote vifuatavyo:

  • Una umri wa miaka 18 au zaidi; na
  • Haupo katika, chini ya udhibiti wa, si raia, au si mkaazi wa: Syria, maeneo ya Crimea, Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhzhia ya Ukraine, Russia, North Korea, Iran, Cuba, au nchi nyingine yoyote au eneo lolote ambalo limezuiwa kufikia huduma na Marekani, Umoja wa Ulaya, au nchi au mamlaka nyingine yoyote;
  • Wewe si “Raia Mteule Maalum” kama ilivyotangazwa na Ofisi ya Kudhibiti Mali ya Kigeni (Office of Foreign Assets Control, “OFAC”) ya Idara ya Hazina ya Marekani au orodha ya vikwazo ya nchi nyingine yoyote, na jina lako lisiwe kwenye Orodha ya Watu Wanaokatazwa ya Idara ya Biashara ya Marekani au orodha za watu waliopigwa marufuku ya nchini nyingine yoyote.

Ikiwa hautimizi vigezo hivi vyote, hauruhusiwi kufikia wala kutumia Huduma, na, ifaavyo, huenda tukazuia uwezo wako wa kufikia au kutumia Huduma.

Aidha, ikiwa uko nchini Ujerumani au makazi yako ya kawaida au ofisi yako rasmi iko nchini humo, hauruhusiwi kufikia wala kutumia huduma za wahusika wengine ilivyofafanuliwa katika Sehemu ya 2.5 au programu bila mamlaka kuu ilivyofafanuliwa katika Sehemu ya 2.8. Vipengele hivi havipatikani kwako.

1.3 Upatikanaji. Kurasa za wavuti zinazoelezea Huduma zinaweza kufikika kote ulimwenguni, lakini hii haimaanishi kwamba Huduma zote au vipengele vyote vya Huduma ni halali au zinapatikana nchini mwako. Ufikiaji Huduma fulani (au vipengele fulani vya Huduma) katika nchi fulani huenda ukazuiliwa nasi au na serikali. Hauwezi kutumia zana za VPN au zana sawa na hizo ili kuepuka vikwazo vyovyote. Ufikiaji Programu, na vipengele fulani ndani ya Programu, huenda ukakosekana au ukawekewa vikwazo, kulingana na eneo lako. Ni wajibu wako kuhakikisha kwamba matumizi yako ya Huduma ni halali mahali ambako unazitumia. Huduma hazipatikani kwa lugha zote.

1.4 Masasisho. Mara kwa mara tunaweza kufanya mabadiliko kwenye Sheria hizi. Tukifanmya hivi, tutaweka sheria zilizosasishwa kwenye Huduma na ambapo inahitajika na sheria husika tutakuarifu kabla ya kufanya mabadiliko yoyote na ambapo mabadiliko hayo huenda yakawa makubwa au yanayokuathiri vibaya, tutakupa ilani ya ziada ya mapema ikiwa inahitajika na sheria husika. Unaelewa na kukubaliana kwamba matumizi yako endelevu ya Huduma baada ya sisi kufanya mabadiliko yoyote kama hayo na ambapo haujakataa mabadiliko hayo inaonyesha kwamba unakubali Sheria zilizosasishwa. Unaweza kuacha kutumia Huduma wakati wowote ikiwa haukubaliani na Sheria hizi. Kwa sababu Huduma zinabadilika kadri muda unavyosonga huenda tukabadilisha au tukasitisha sehemu ya Huduma au Huduma zote, wakati wowote na bila ilani, kwa hiari yetu pekee, kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria husika.

1.5 Sheria za Ziada. Sheria na masharti ya ziada huenda yakatumika kwa matumizi, maudhui, vipengele, au sehemu maalum za Huduma, na sheria na masharti hayo yote ya ziada tutakayokupatia yatakuwa sehemu ya Sheria hizi.

2. Huduma

2.1 Pochi la Bila Umiliki. Programu ya World inajumuisha pochi la bila umiliki la kuhifadhia sarafu za kidijitali zinazoruhusiwa au mali ya kidijitali (ikijumuisha WLD na kwa pamoja, “Sarafu za Kidijitali”). Unadhibiti Sarafu za Kidijitali zilizo ndani ya pochi lako. Unapotumia Programu ya World, funguo za kibinafsi (ambazo ni manenosiri ya kufikia Sarafu hizo za Kidijitali) zinahifadhiwa moja kwa moja kwenye kifaa chako. Wakati wowote, kulingana na uwepo wa intaneti na msongamano kwenye blockchain, unaweza kutoa Sarafu zako za Kidijitali kwa kuzituma kwenye anwani tofauti ya blockchain. Unapohifadhi Sarafu zako za Kidijitali ndani ya pochi lako hatuna udhibiti juu ya pochi lako, Sarafu zako za Kidijitali, au funguo za kibinafsi. Watumiaji wanawajibikia hasara ya kupoteza funguo zao za kibinafsi na TFH wala Programu ya World haziwezi kurejesha funguo hizo.

Kwa sababu Programu ya World ni pochi liliso na umiliki, utapatiwa anwani ya pochi ambayo inabainisha ni wapi Sarafu zako za Kidijitali zimehifadhiwa kwenye blockchain husika. Hatuna uwezo wa kufikia Sarafu zako za Kidijitali.

2.2 Sarafu za Kidijitali Zinazoruhusiwa. Programu ya World inaruhusu sarafu fulani za ERC-20. Tunaweza kuruhusu Sarafu za Kidijitali za ziada katika siku zijazo. Programu ya World inaonyehsa Sarafu za Kidijitali zinazoruhusiwa. Hakikisha kukagua ni sarafu na mitandao gani inaruhusiwa ndani ya Programu ya World kabla ya kuweka na kutoa Sarafu zako za Kidijitali. Ukituma sarafu zisizoruhusiwa kwenye anwani ya pochi isiyo sahihi hatuna uwezo wa kurejesha Sarafu zako za Kidijitali.

Unaelewa kwamba kutuma Sarafu za Kidijitali zisizoruhusiwa kwenye anwani ya pochi la Programu ya World kunaweza kumaanisha utapoteza kabisa uwezo wa kufikia Sarafu hizo za Kidijitali. Hatuna njia ya kufikia Sarafu za Kidijitali. Tafadhali hakikisha unatuma Sarafu sahihi za Kidijitali kwa anwani sahihi ya pochi nyakati zote. Unaweza kufanya muamala wa majaribio ukitumia kiwango kidogo cha Sarafu za Kidijitali.

2.3 Utoaji na Ufikiaji. Unapotangamana na Sarafu zako za Kidijitali - kama vile kuzituma hadi kwenye anwani nyingine ya pochi au kuunganisha na programu iliyotolewa - ukitumia Huduma, utahitajika kuidhinisha au “kutia sahihi” utangamano huo kupitia vifaa ambavyo umetambulisha wakati wa mchakato wa usajili. Programu zinategemea kikamilifu idhini zako kwenye vifaa hizi ili kuanzisha utangamano na blockchain husika. Unaelewa kwamba unatangamana moja kwa moja na blockchain husika unapofanya utangamano huu na kwamba hatuwajibikii uwasilishaji oda kwa niaba yako.

2.4 Maelezo kuhusu Wahusika Wengine. Kwa kutumia Huduma huenda ukafikia maelezo kuhusiana na Sarafu zako za Kidijitali, kama vile, lakini sio tu, thamani yake ya sasa sokoni. Uwasilisho wa maelezo haya hakuashirii ushirikiano au uungaji mkono wowote wa wahusika wengine, hata ikiwa utendaji fulani unaotolewa kuhusiana na Huduma unahitaji matumizi ya bidhaa hizo za wahusika wengine. Maudhui ya huduma na bidhaa hizo za wahusika wengine kama ilivyotajwa kupitia Huduma yanategemea maelezo yaliyowekwa hadharani au na wahusika hao wengine kwetu, na kwa hivyo hatutoa uwakilisho au kutoa hakikisho kuhusu usahihi wa maelezo yanayohusiana na huduma au bidhaa za wahusika wengine.

2.5 Huduma za Wahusika Wengine

Watumiaji wanaoishi nchini Ujerumani au makazi yao ya kawaida au ofisi yao rasmi iko nchini humo, hawawezi kutumia Huduma za Wahusika Wengine ili kuuza au kubadilishana Sarafu zao za Kidijitali chini ya Sehemu hii.

Zinakopatikana, Huduma zinaweza kukupa viungo elekezi vya vichakataji vya wahusika wengine ili kuchakata miamala kama vile ununuzi wa Sarafu za Kidijitali kwa kutumia pesa za kawaida, uuzaji Sarafu za Kidijitali, ubadilishanaji Sarafu za Kidijitali, na utendaji mwingine ambao unaweza kuwepo katika siku zijazo. Unaweza kuona ni huduma gani za wahusika wengine zinapatikana ndani ya Programu ya World. Unapofanya miamala hii, unafanya miamala na wahusika wengine na si sisi. Ni lazima ufuate maagizo husika yanayotokewa mtoa huduma mwingine na ukubali sheria zao za huduma. Hatuchukui udhibiti wala kutuma fedha zako au Sarafu za Kidijitali wakati wowote tunapotoa Huduma zetu, au wakati unatumia huduma za wahusika wengine.

2.6 Miamala ya Mtu-kwa-Mtu. Huduma zinatoa jukwaa la mawasiliano kwa ambalo unaweza kutuma, kuomba, kupokea, na kuhifadhi Sarafu za Kidijitali zinazoruhusiwa kutoka kwenye, mapochi mengine ya blockchain, iwe unayadhibiti au ni ya wahusika wengine. Utumaji wako wa Sarafu za Kidijitali zinazoruhusiwa kati ya anwani nyingine zako za blockchain na hadi na kutoka kwa wahusika wengine ni utumaji. Mtu anayeanzisha muamala huo anawajibikia pekee yake utekelezaji muamala kwa nija inavyofaa, inayojumuisha, miongoni mwa mambo mengine, malipo ya ada tosha za mtandao au wathibitishaji ili muamala kufaulu. Ada za mtandao zisizotosha zinaweza kusababisha utumaji kusalia katika hali ya bila kukamilika (pending) na kunaweza kusababisha kuchelewa au hasara kutokea kwa ajili ya hitilafu katika kuanzisha muamala. Hatuna jukumu la kusaidia katika usuluhishaji miamala hiyo. Unapotuma Sarafu zozote za Kidijitali kutoka kwa pochi lako hadi pochi nyingine la blockchain, utumaji huo unautekeleza ndani ya blockchain na hatuna udhibiti. Unapaswa kuthibitisha maelezo yote ya muamala kabla ya kuyawasilisha. Hatuchukui dhima au wajibu endapo utaweka anwani pokezi isiyo sahihi ya blockchain. Utumaji Sarafu za Kidijitali hauwezi kughairiwa baada ya kuwasilishwa kwenye mtandao wa blockchain husika, ingawa huenda ikawa katika hali ya kusubiri, na kuchakatwa ifaavyo, huku miamala ikichakatwa na waendeshaji mtandao. Hatudhibiti mtandao na hatutoi hakikisho kwamba utumaji utathibitishwa na mtandao.

2.7 Vault

2.7.1 Taarifa za Jumla. Programu ya World hutoa njia ya kufikia "vault" bila mamlaka kuu ya Sarafu zako za Kidijitali ("Vault"). Matumizi yako ya Vault yanajumuisha kutambua kwako na kukubali sheria na masharti yanayosimamia Vault, pamoja na masharti yoyote ya ziada yaliyotolewa na wahusika wengine ambao wametengeneza au kutoa vipengele vinavyohusiana au vinavyotokana na matumizi yako ya Vault.

Vault inatumia Sarafu fulani za Kidijitali pekee. Sarafu hizi za Kidijitali hazistahili kuwa Sarafu Zinazochukuliwa kama Mali au Sarafu za E-Money, kwa masharti yaliyowekwa na Kanuni ya (EU) 2023/1114 ya Bunge la Ulaya na Baraza la tarehe 31 Mei 2023 kwenye masoko ya mali ya crypto. Sarafu za Kidijitali zinatumika zitaonyeshwa katika World App unapoingia kwenye Hazina yako. Sarafu za Kidijitali zinazotumika na Vault zinaweza kubadilika mara kwa mara, na hakuna hakikisho kwamba Sarafu za Kidijitali zinazotumika zitaendelea kupatikana kwa matumizi katika Vault.

Vault hutolewa kwa uhusiano na mikataba ya wahusika wengine mahiri. Hakuna mtu mwingine au shirika, kando na wewe, lililo na uwezo wa kuingiliana na Vault yako au Sarafu za Kidijitali ndani ya Vault yako. TFH wala mhusika mwingine hawana funguo za usimamizi au ufikiaji (fursa au vinginevyo) kwa Vault yako au mikataba mahiri husika. Kuweka Amana kwenye, au kutoa kutoka kwa, Hifadhi ya Sarafu zozote za Kidijitali za akaunti yako kunaweza tu kutokea ikiwa shughuli kama hiyo imetiwa sahihi kwa ufunguo wako wa faragha unaolingana uliofafanuliwa katika Sehemu ya 2.1 ya Sheria na Masharti haya. Hii ina maana kwamba ukipoteza ufikio au udhibiti wa ufunguo wako wa faragha, hutaweza kuweka amana au kutoa Sarafu za Kidijitali zozote kutoka kwa Vault na hakuna mhusika mwingine atakayeweza kukusaidia au kufanya hivyo kwa niaba yako kwenye kifaa chako. Ipasavyo, matumizi ya Vault hayatoi, na hayawezi, kukupa ulinzi wowote, dhamana, au huduma za uhamisho na TFH au mtu mwingine yeyote kuhusiana na Sarafu zozote za Kidijitali unazoweza kuzifunga kwa kutumia Vault kwenye akaunti yako.

Mkataba mahiri unaosimamia utendakazi wa Vault kwa sarafu za WLD unaweza kutazamwa kwa kutumia blockchain hapa. Kwa ajili ya uwazi, matumizi ya vipengele hivi na vingine vyovyote vinavyohusiana na Vault yako chini ya Kanusho lilelile la Dhima lililo katika Sehemu ya 12 ya Masharti haya.

2.7.2 Utendaji wa Vault. Vault kwa sasa inatoa vipengele vifuatavyo, ambavyo vinaweza kubadilishwa, kuondolewa au kuongezwa na TFH au wahusika wengine: Kufunga, Mazao, Kipindi cha Uondoaji na Usalama, Ruzuku kwenye Vault.

2.7.3 Kufunga. Kwa kutumia Vault, unakubali kufunga Sarafu zako za Kidijitali kwa muda uliowekwa. Kufunga Sarafu za Kidijitali kwa kutumia Vault yako kutahamisha Sarafu hizo za Kidijitali kutoka kwa mkoba wako usio na dhamana hadi kwenye kandarasi mahiri iliyogatuliwa. Baada ya kuhamishwa, Sarafu hizi za Kidijitali "zitafungwa" kwenye vault, wakati ambapo inajumuisha kipindi ambacho zinasalia kuhifadhiwa kwenye Vault pamoja na muda ulioamuliwa mapema unaoitwa "Kipindi cha Usalama," ambacho kimefafanuliwa kwa undani zaidi hapa chini. Ingawa Sarafu zako za Kidijitali zimefungwa, hutaweza kufikia, kuhamisha au kufanya muamala mwingine wowote ukizitumia hadi utakapoomba kuziondoa na kuruhusu Kipindi kinachotumika cha Usalama kupita. Hakuna yeyote, ikiwemo TFH au Mtoa Huduma mwingine, aliye na uwezo wa kufungua, kuhifadhi, kudhibiti, kutoa au kuhamisha Sarafu zako za Kidijitali zilizofungwa. Kuweka Sarafu zako za Kidijitali kwenye Vault na kuziwekea vikwazo vya kufunga na kuziondoa hakujumuishi mauzo, mkopo, au uhamisho wa haki zozote, hatimiliki au riba katika Sarafu za Kidijitali kwa TFH au mtu mwingine yeyote.

Kufunga Sarafu zako za Kidijitali kwenye Vault hakukuhakikishii ulinzi au ulinzi wa Sarafu zako za Kidijitali. Hakuna mpango wa bima ya amana, au ulinzi wowote kama huo, unaotumika kwa Sarafu zako za Kidijitali, na thamani na/au matumizi ya Sarafu zozote za Kidijitali ulizofunga zinaweza kuongezeka au kupungua katika muda wote wa Kipindi cha Usalama. Hii inamaanisha kuwa thamani au matumizi ya Sarafu zozote za Kidijitali utakazofungia kwenye Vault yako zinaweza kupungua, au kwenda hadi sifuri katika Kipindi cha Usalama. Unakubali na kukubali kwamba uondoaji wowote wa Sarafu za Kidijitali kwenye akaunti yako baada ya Kipindi kinachotumika cha Usalama kunaweza kusababisha kurejeshwa kwa Sarafu za Kidijitali ambazo zina thamani ya chini, au zisizo na thamani, kuliko zilivyokuwa wakati ukizifunga kwenye Vault yako, na. kwamba TFH au wahusika wengine watabeba hatari au wajibu wa kupunguzwa kwa thamani yoyote ambayo inaweza kutokea.

2.7.4 Mazao. Unaweza pia kustahiki kuzalisha kile, kwa madhumuni ya bidhaa hii, kinajulikana kama "mazao" kwenye Sarafu fulani za Kidijitali kwenye Vault yako. Mazao haya, ambayo yanaweza kuchukua muundo wa Sarafu za ziada za Kidijitali, hutolewa na mtu mwingine kupitia mfululizo tofauti wa utendakazi mahiri wa mikataba ambayo unaweza kufikia kwa kutumia kiolesura kilichotolewa ndani ya World App. Hakuna TFH wala mtu mwingine yeyote anayetumia, kuchukua udhibiti, kupokea amana yoyote kwa, au kutupilia mbali Sarafu zako za Kidijitali. Kwa hivyo, mazao si riba ambayo inahusishwa au kuzalishwa na kitu chochote isipokuwa kufunga Sarafu zako za Kidijitali kulingana na sheria na masharti yaliyotolewa. Mazao yoyote ambayo unaweza kupokea yametolewa kwako kama ruzuku na mtu mwingine kulingana na maamuzi yako ya kuhifadhi Sarafu za Kidijitali kwa kutumia Vault. Vigezo vinavyobainisha uzalishaji wa mazao, ikijumuisha kiasi kinachozalishwa au muda ambao yanaweza kuongezeka, vinaweza kubadilishwa au kughairiwa wakati wowote, kwa hiari ya Mtoa Huduma mwingine.

Kunaweza kuwa na kiwango cha juu cha mazao unachoweza kupata. Maelezo haya yataonyeshwa kando ya Vault yako na kupitia sheria na masharti yoyote ya ziada yaliyotolewa na mtu mwingine (anayetambuliwa kama "Mtoa huduma" ndani ya World App) anayetoa mazao. Masharti haya ya ziada pia yamejumuishwa katika Masharti haya. Mazao hayatolewi au kuhudumiwa na TFH.

Mazao yoyote yatakayopatikana yatasambazwa kwako tu baada ya kukamilika kwa uondoaji kwa Sarafu zozote za Kidijitali zinazozalisha mazao kutoka kwa Vault, ambayo hutokea tu baada ya Kipindi chochote cha Usalama kinachotumika kuisha. Uondoaji huu ni sharti la mwisho la ruzuku yoyote ya mazao, kumaanisha kuwa huna haki, hatimiliki au riba katika mazao yoyote ambayo yamezalisha au yatakayotolewa isipokuwa na hadi wakati ambapo mazao yamepokelewa katika mkoba wako usio na dhamana. Hii pia inamaanisha kuwa ukipoteza ufikio au udhibiti wa ufunguo wako wa faragha, hutaweza kutoa pesa zozote ambazo zitakupa haki ya kupokea mazao.

2.7.5 Kipindi cha Uondoaji na Usalama. Unaweza kuanzisha uondoaji wa Sarafu zako za Kidijitali kutoka kwa Vault yako wakati wowote. Sarafu za Kidijitali ambazo umeomba kuondoa kwenye Vault yako zitarejeshwa kwako baada ya muda uliowekwa awali unaoitwa "Kipindi cha Usalama" kupita. Kila wakati unapoanzisha uondoaji wa Sarafu za Kidijitali kwenye Vault, Kipindi kipya cha Usalama kitaanza na kuhesabu muda hadi Sarafu hizo za Kidijitali zitakaporejeshwa kwako. Wakati huu, Sarafu za Kidijitali ulizochagua kuondoa zitasalia zimefungwa, na unaweza pia kughairi uondoaji wako. Baada ya Kipindi cha Usalama kupita, uondoaji wako utakamilika na Sarafu za Kidijitali, pamoja na mazao yoyote ambayo huenda yamepatikana, yatatumwa kwenye mkoba wako. Muda wa Kipindi cha Usalama utabainishwa ndani ya World App utakapofikia Vault yako.

2.7.6 Ruzuku kwenye Vault. Kipengele hiki, kikichaguliwa, hukuwezesha kutuma kiotomatiki Ruzuku za WLD moja kwa moja kwenye Vault kwenye akaunti yako badala ya kwenye pochi yako. Unaweza kubadilisha mpangilio huu wakati wowote.

2.7.7 TFH na Vault. Ufikiaji kipengele hiki kunafanywa kupitia World App. Hata hivyo, TFH itaweza tu kusoma data husika na kuionyesha kwako. TFH haiwezi kuhamisha, kuondoa au kuweka Sarafu zako za Kidijitali na haina ufikio wowote kwa Vault yako.

2.8 Programu Bila Mamlaka Kuu

Sehemu hii haitumiki kwa watumiaji walio nchini Ujerumani au wale ambao makazi yao ya kawaida au ofisi yao rasmi iko nchini humo:

Zinakopatikana, huenda tukawa na utendaji unaokuwezesha kuunganisha pochi lako na programu mbalimbali bila mamlaka kuu. Una wajibu wa kuhakikisha usalama wa programu hizi za wahusika wengine. Hatudhibiti programu za wahusika wengine na hatuwezi kutoa usaidizi kwa ajili ya matatizo yoyote unayoweza kupata unapounganisha na programu za wahusika wengine.

2.9 Huduma kwa Wateja. Tunatoa usaidizi kwa wateja kuhusu vipengele na utendaji fulani unaohusiana na Huduma. Ili kuwasiliana nasi, chagua “Usaidizi” kwenye menyu ya ndani ya programu au kupitia anwani [email protected].

2.10 Kiolesura cha World ID. Asasi ya Worldcoin Foundation, na si TFH, inaongoza Teknolojia ya World ID na kudhibiti uchakataji wa data zinazohusiana na kifaa cha Orb ili kuthibitisha World ID. Tunaweza kufanya World ID yako kupatikana kwako (kama kiolesura) kupitia Huduma. Teknolojia ya World ID inakuwezesha kuthibitisha kwamba wewe ni binadamu wa kipekee huku ikilinda faragha yako.

2.11 Mpango wa Kualika. Inakopatikana, tunaweza kufanya huduma ya ‘Kualika’ kupatikana kwako. Kwa kutumia huduma ya Kualika, unaweza kuwaalika marafiki na familia wapakue Programu ya World na wathibitishwe ili kupata World ID. Ikiwa unatumia huduma ya Kualika unakubaliana na sheria na masharti yafuatayo:

Zawadi kwa ajili ya kushiriki kwenye huduma ya Kualika zinatolewa na World Assets Limited. World Assets Limited, kwa hiari yao, wanaweza kukupa zawadi kwa ajili ya kuwaalika watumiaji ambao wanafanikiwa kuthibitisha World ID yao. Ili kupokea zawadi hii, ni lazima utimize masharti fulani, ambayo utaelezewa kwenye Programu ya World. Una kipimo cha ni watumiaji wangapi unaweza kupendekeza kwenye Programu ya World. Kipimo hiki kimeonyeshwa kwenye Programu ya World.

Hauhitaji kufanya ununuzi wowote ili kushiriki katika kipengele cha Kualika. Huduma ya Kualika inapatikana tu kwa matumizi ya kibinafsi na yaisyo ya kibiashara. Unaweza tu kutumianhuduma ya Kualika kwa nia nzuri ya malengo ya kisheria. Hauwezi: (a) kutumia huduma ya Kualika au Huduma kwa nia ya udanganiyifu, ulaghai au isiyo ya kisheria; (b) kufanya kitu chochote kuharibu bioashara, nia au sifa yetu; (c) kuwasilisha matangazo au nyenzo za kimatangazo bila idhini; (d) kufanya madai ya uwongo au ya kupotosha; (e) kutumia utafutaji wa kulipiwa, midia ya kulipiwa au shughuli nyingine sawa ili kuwashawishi watumiaji kupitia huduma ya Kualika; na (f) kutumia huduma ya Kualika ili kujaribu kupata maelezo ya kibinafsi kutoka kwa watumiaji wengine.

Huduma ya Kualika haipatikani katika nchi zote au maeneo yote na haipatikani kwa watumiaji wote. Ushiriki katika huduma ya Kualika haupatikani katika mamlaka yoyote ambapo huduma hii yote au sehemu yake huenda inakiuka (au kutufanya kukiuka) mahitaji yoyote ya kisheria. Unakubali kutotumia huduma ya Kualika ikiwa huduma ya Kualika haiambatani na sheria husika katika eneo lako.

Huduma ya Kualika inapatikana kwa hiari yetu pekee. Tunaweza kubadilisha, kurekebisha, kusimamisha na kubatilisha huduma hii wakati wowote. World Assets Limited, kwa hiari yao, wanaweza kukataa kukupa zawadi kwa ajili ya kuwaalika watumiaji kuthibitisha World ID yao pale ambapo wamekiuka Masharti haya.

2.12 Ruzuku za WLD na Uhifadhi Ruzuku za WLD. Mojawapi ya huduma za Wahusika Wengine inachukua kiwango kidogo cha WLD katika nyakati tofauti (“Ruzuku za WLD”). Ruzuku za WLD zinatolewa na kampuni ya World Assets Limited, kampuni tanzu ya asasi ya Worldcoin Foundation. Viwango, mipishano, na mida haswa ya Ruzuku za WLD zitabainishwa kwenye Programu ya World, lakini zinaamuliwa pekee na World Assets Limited. Ikiendana na matoleo ya hapo mbeleni ya sheria hizi, Uhifadhi Ruzuku za WLD uliopo hautoi hakikisho kwamba utapokea kiwango chochote cha Ruzuku za WLD. Viwango, mipishano, na mida haswa ya Uhifadhi Ruzuku za WLD zitabainishwa kwenye Programu ya World, lakini zinaamuliwa pekee na World Assets Limited. Uhifadhi wa Ruzuku za WLD unaweza kuishiwa na muda, kwa ilani au bila ilani kwenye Programu ya World, bila kujalisha kama tayari umefanya Uhifadhi wa Ruzuku za WLD au umepokea Ruzuku husika ya WLD. Inaweza kubatilishwa kwa hiari ya World Assets Limted.

2.13 Programu ya Operator. Wahudumu wa Orb na washirika wengine tunawapa Programu ya Operator inayowawezesha kufuatilia shughuli na takwimu fulani zinazowahusu nyinyi na biashara zenu kama Wahudumu wa Orb. Pia tunaweza kuweka vipengele fulani vya kukusaidia kuendesha biashara zenu kama Wahudumu wa Orb.

2.14. Miniapps. “Miniapps” ni kipengele cha Programu ya World kinachokuwezesha kufikia mfumo wa programu ndogo ambazo zinaweza kufikiwa ndani ya Programu ya World. Ni kwa hiari yetu pekee tunabainisha jinsi Miniapps zinaonyeshwa ndani ya Programu ya World. Ni lazima uwe na anwani ya pochi la Programu ya World ili kutumia Miniapps.

Inatambua kwamba katika kuonyeshana Miniapps, TFH inatoa mfumo wa teknolojia inayowaunganisha watumiaji pekee. Hakuna wakati TFH inatuma, kuhifadhi, kuchukua umiliki, kumiliki, au vinginevyo kujihusisha na rarafu yoyote ya kawaida au kidijitali.. TFH haichakati miamala, kutenda kama mnchakataji malipo, au vinginevyo kuhusika katika kuchakata miamala. TFH si mhusika kwenye miamala na hana dhima kuhusiana na miamala hii. TFH haiwezi kutoa usaidizi kuhusiana na matatizo kwenye miamala.

2.14.1 Miamala na Malipo kuhusiana na Miniapps. Miniapps zinaonyeshwa ndani ya Programu ya World na zinaweza kutoa bidhaa au huduma ambazo watumiaji wa Programu za World huenda wakanunua wakitumia Sarafu za Kidijitali kwenye mapochi yao ya Programu ya World. Miamala hii inafanyika kati yako na miniapp husika. TFH si mhusika kwenye muamala wowote kama huo.

Kuhusiana na miamala yoyote kama hiyo, unatambua kwamba pochi la Programu ya World ni huduma ya kutomiliki, a,mayo TFH jaihifadhi wala kumiliki Sarafu zako za Kidijitali na haifanyi miamala, kutuma, kumiliki, au vinginevyo kuhusika kwa njia yoyote katika kufanya miamala yoyote. Sarafu za Kidijitali kila wakati zinahifadhiwa na kutumwa kwenye mitandao husika ya blockchain. Hakuna hakikisho kwamba miamala itachakatwa kwa njia sahihi.

TFH inakupatanisha wewe na mhusika mwingine kwenye mfumo wa Miniapps na si mhusika kwenye miamala yoyote. TFH hainajukumu lolote katika uchakataji malipo na kusimamia urejeshaji fedha wala ada za kughairi.

Unapoamua kujihusisha katika muamala, ni lazima utume kiwango kilichokubalianwa na aina ya Sarafu za Kidijitali. TFH haichakati Sarafu za Kidijitali au za kawaida za mtumiaji na haifanyi utumaji wowote kwa niaba ya watumiaji. TFH haishughulikii, kudhibiti, kusimamia, kuthibitisha wala kutoa hakikisho lolote kuhusu miamala yoyote. Endapo muamala haujapokea, umerejeshwa, umechakatwa vibaya, au vinginevyo umekumbwa na hitilafu, wewe na watoa huduma hao wengine ni lazima mshirikiane ili kusuluhisha suala lolote. Migogoro, madai, hasara, kutoelewana, hitilafu za kiufundi, au masuala yoyote ya aina yoyote (ya kiajali na yanayodaiwa kuwa ya kimakusudi) yanayohusiana na malipo au miamala ni lazima yashughulikiwe moja kwa moja kati yako na mtoa huduma huyo mwingine. TFH haina wajibu wowote na haitahusika katika migogoro au majadiliano yoyote yanayohusiana na malipo, na haina dhima kwa hasara zozote ambazo huenda zikakumba wahusika.

Unawajibika pekee yako katika kukubali hatari ya mabadiliko yoyote ya bei kuhusiana na thamani ya Sarafu za Kidijitali, na unaelewa kwamba kufikia wakati unapokamilisha muamala, thamani ya Sarafu za Kidijitali zinazohusika kwenye muamala huenda ikawa imebadilika pakubwa.

2.14.2 Wahusika Wengine. Bidhaa na huduma zinazoonyeshwa kwenye miniapp yoyote zinatolewa na kudhibitiwa na wahusika wengine. Kwa kutumia miniapps, unatambua na kukubaliana kwamba:

  • Sheria hizi ni kati yako na sisi, na sio na miniapp yoyote maalum;
  • Unatumia programu iliyotengenezwa na/au kutolewa na programu ya mhusika mwingine, ambayo mhusika huyo anawajibikia miniapp hiyo;
  • TFH inawezesha tu kufikia watoa huduma za malipo wengine kupitia pochi la Programu ya World, na wao wenyewe hawachakati malipo wala kuhifadhi fedha;
  • Miniapps zinaweza kuwa na masharti ya ziada kama sehemu ya bidhaa au huduma zao kwa ambazo ni lazima ufuate ikiwa unakubali huduma yao; na
  • Unatambua kikamilifu na kukubali hatari zozote na zote zinazohusiaba a miamala, na unakubali kwamba hatutakuwa na dhima kwa hatari zozote au madhara yoyote mabaya yanayoibuka kutokana na miamala hiyo.

Watengenezaji binafsi wa miniapps zinazopatikana kwenye Miniapps wanawajibikia maudhui, bidhaa, au huduma zinazopatikana kwako moja kwa moja kupitia miniapps zao husika. Ikiwa una maswali au migogoro yoyote utawasiliana na na Mtengenezaji husika moja kwa moja.

Watumiaji wanakubali hatari zote zinazohusiana na kufanya muamala, pamoja na hatari kwmba hawatapokea mapato ya uuzaji au ununuzi wao. Endapo kutakuwa na tatizo kuhusiana na muamala wowote, TFH haitaweza kusaidia katika kusuluhisha, wala kuwa na dhima yoyote kwa ajii ya matatizo yanayoibuka kutokana na miamala yoyote.

2.14.3 Ada za TFH. Huenda tukaongeza ada za kutumia Miniapps unapofanya muamala na Mtengenezaji. Utaonyeshwa kiwango cha ada hii ndani ya mfumo. Ada zote zinaonyeshwa na ni za sasa kama inavyoonyeshwa kwenye Miniapps na huenda zikasasishwa na kubadilishwa mara kwa mara.

2.14.4 Ushuru. Ni wajibu wako kubaini kama, na kwa kiwango gani, ushuru unatumika kwa muamala wowote kupitia Miniapps au miamala yoyote unayofanya pale, na kushikilia, kuchukua, kuripoti na kuwasilisha kiwango sahihi cha ushuru kwa mamlaka mwafaka za ushuru.

2.14.5 Hakuna usimamizi kwa ujumla. TFH haitakuwa na jukumu jumla la kufuatilia maelezo yanayosambazwa na watumiaji, wala haitachambua maelezo au hali zinazoonyesha shughuli haramu ndani ya Miniapps.

Hata hivyo, tukifahamu, bila kujalisha mbinu iliyotumiwa, kwamba bidhaa au huduma haramu imetolewa kupitia Miniapps kwa watumiaji wanaoishi katika Umoja wa Ulaya, tutawafahamisha watumiaji hao kwamba wamenunua bidhaa au huduma haramu kupitia Miniapps.

2.14.6 Shughuli Ziilizopigwa Marufuku. Watumiaji wa Huduma za Miniapps wanakubali kutochapishaau kusambaza maudhui yoyote yanayokiuka sheria zozote au kukiuka haki zozote za mhusika mwingine, ukijumuisha lakini sio tu haki zozote za mali bunifu, haki zozote za faragha, au haki zozote za kutangazwa.

Pia, unakubali kutojihusisha katika shughuli zozote ambazo:

  • Ni haramu, za ulaghai, au zinadhuru;
  • Zinahitilafiana au kudakiza uendeshaji Miniapps;
  • Zinakiuka sheria zozote zilizobainishwa kwenye Mwongozo wetu wa Programu; na
  • Zinajumuisha maudhui ambayo hayajaruhusiwa chini ya Mwongozo wa Programu.

2.14.7 Kuripori maudhui haramu. Programu ya World ina mbinu rahisi kufikia za watumiaji kuwasiliana nasi kuhusu maudhui haramu katika jukwa la Miniapps. Tutachukua hatua ya haraka ili kukagua ripoti hizo.

2.14.8 Kuondoamaudhui haramu. Tukibaini kwamba miniapp yoyote ina maudhui haramu au inatoa bidhaa au huduma haramu, miniapp hiyo itaondolewa kwenye Miniapps. TFH itatoa kauli fupi, wazi na maalum kuhusu sababu kwa mchapishaji yeyote wa maudhui au huduma haramu.

Vikwazo vyovyote vinavyotekelezwa na Programu ya World dhidi ya watumiaji wake vitatekelezwa kwa heshima, haki na kiwango kinachofaa.

Watumiaji wanaoamini kwamba maudhui yao yameondolewa au ufikiaji wake kulemazwa kwa njia isiyo ya haki wanaweza kuwasiliana nasi kupitia [email protected] ili kukata rufaa kuhusu uamuzi huo. Tunatoa mfumo wa malalamishi wa kielektroniki na wa bila malipo unaowawezesha watumiaji kupinga maamuzi yetu yanayohusiana na maudhui kuondolewa, huduma kusitishwa, akaunti kufungwa, au vikwazo vya fedha kwa ajili ya madai ya maudhui haramu au ukiukaji sheria.

2.14.9 Kudhibiti Maudhui. TFH inahifadhi haki za kusitisha, kwa kipindi cha muda na baada ya kupeana onyo ya mapema ambapo inahitajika kufanya hivyo kisheria, utoaji wa huduma zetu kwa watumiaji ambao mara nyingi wanatoa maudhui haramu. TFH pia kwa muda inaweza kusitisha uchakataji wa ilani na malalamishi kutoka kwa watumiaji ambao mara nyingi wanawasilisha madai bila ushahidi.

2.15. Majina ya Watumiaji. Jina lako la mtumiaji la Programu ya World si lazima liwe jina lako halisi. Unapochagua jina la mtumiaji una jukumu la kufuata Sera ya Jina la Mtumiaji kwenye toleo lake mpya kabisa.

3. Ununuzi, Ada, na Ushuru

3.1 Ada za Miamala. Kwa kutumia Huduma, unakubali kulipa ada zote husika pamoja na ada za miamala ya kubadilishana Sarafu za Kidijitali na miamala. Tutakuarifu kuhusu ada zozote husika kabla ya kufanya muamala. Ikiwa wewe ni huduma ya malipo ya mhusika mwingine, ada za benki, ada za kadi ya mkopo, ada za kadi ya salio zinazotozwa kwa ajili ya ununuzi wowote wa Sarafu za Kidijitali huenda zikaongezwa kwenye kiwango cha malipo unayolipia ununuzi wako wa Sarafu za Kidijitali. Pia unawajibikia ada zozote za ziada zinazotozwa na mtoa huduma za kifedha kwako.

3.2 Ada ya Mtandao. Utangamano na blockchain pia unatoza ada ya mtandao. Ada ya mtandao inatozwa na kulipwa kwenye mtandao wa blockchain, na sio sisi, kwa kuwezesha utangamano wowote. Katika baadhi ya matukio, unaweza kustahiki kupata idadi ndogo ya miamala bila ada katika kipindi fulani kinachoamuliwa na TFH kwa hiari. Miamala hiyo inawekewa thamani ya chini zaidi ya miamala ambayo TFH inaweza kubadilisha.

3.3 Ushuru. Ni wajibu wako kubaini kama, na kwa kiwango gani, ushuru unatumika kwa muamala wowote kupitia Huduma, na kushikilia, kuchukua, kuripoti na kuwasilisha kiwango sahihi cha ushuru kwa mamlaka mwafaka za ushuru.

3.4 Masasisho. Ada zote zinaonyeshwa na ni za sasa kama inavyoonyeshwa katika Huduma na huenda zikasasishwa na kubadilishwa mara kwa mara.

4. Vipengele vya Hatari

4.1 Si Sarafu Rasmi Kisheria. Sarafu za Kidijitali si sarafu rasmi kisheria, na haziungwi mkono na serikali yoyote, na akaunti za Sarafu za Kidijitali na salio la thamani kwenye Huduma haziko chini ya ulinzi wa Federal Deposit Insurance Corporation, Securities Investor Protection Corporation, au ulinzi kama huo ulio katika nchi nyingine. Sisi si benki na hatutoi huduma za kifedha. Miamala inayofanywa kwenye Programu ya World haidhibitiwi katika nchi nyingi. Hatutoi hakikisho lolote kuhusiana na utendaji wa blockchain tunayotumia, ambayo, miongoni mwa mambo mengin, inaweza kuchelewa, kuwa na ukinzani wa nia, au maamuzi ya kioperesheni kutoka kwa wahusika wengine ambayo si ya kuridhisha kwa wamiliki fulani wa Sarafu za Kidijitali, au kupelekea wewe kutoweja kukamilisha muamala ukitumia Huduma. Muamala unaowasilisha kupitia Huduma huenda ukakosa kukamilika, au huenda ukacheleweshwa pakubwa kwenye blockchain husika, na hatuwajibikii muamala kukosa kuthibitishwa au kusindikwa kama invyotarajiwa. Hakuna waranti wala hakikisho kwamba utumaji unaofanywa kupitia Huduma utafanikiwa kuhamisha umiliki au haki za Sarafu yoyote za Kidijitali. Aidha, kunaweza kuwa na hatari zinazohusiana na matumizi fulani ya Sarafu za Kidijitali, kama vile WLD. Maelezo zaidi kuhusu hatari zinazohusishwa haswa na WLD yanaweza kupatikana hapa.

4.2 Teknolojia Mpya. Huduma ni mpya. Ingawa programu hii imefanyiwa majaribio ya kina, programu inayotumika kwenye Huduma bado ni mpya na huenda ikasa na kasoro au hatari za kisualama. Adja, bado programu inatengenzwa na huenda ikapitia mabadiliko makubwa kadri muda unavyosonga ambayo huenda yakakosa kutimiza matarajio ya watumiaji.

4.3 Hatari ya Uaslama wa Maelezo. Sarafu za Kidijitali na matumizi ya Huduma huenda yakakumbwa na udukuzi au wizi. Wadukuzi au makundi au mashirika mengine yenye nia mbaya yanaweza kuhitilafiana na Huduma kwa njia mbalimbali, ikijumuisha, lakini sio tu, mashambulizi ya malware, mashambulizi ya kukataza huduma, mashambulizi ya kiidhini, mashambulizi ya Sybil, uporaji fedha kwa viwango vidogo vidogo na ulaghai wa kujifanya mtu mwingine ili kutekeleza wizi. Aidha, kwa sababu mitandao ya blockchain tunayoruhusu, kama vile mtandao wa Ethereum, inatumia programu ya “open-source”, programu ambayo ndio msingi wa Huduma huenda ikawa na kasoro za kimakusudi au zisizo za kimakusudi ambazo huenda zikaathiri vibaya Huduma au kupelekea upotezaji a Sarafu za Kidijitali za mtumiaji au mtumiaji kushindwa kufikia au kudhibiti pochi lake kupitia Huduma. Endapo kutakuwa na kasoro kama hiyo ya programu, huenda kukawa hakuna suluhu na watumiaji hawahakikishiwi suluhu yoyote, kurejeshewa fedha au fidia.

4.4 Usahihi. Ingawa tunakusudia kutoa maelezo sahihi na kwa wakati yanayotolewa kupitia Huduma (ikijumuisha, bila kipimo, maudhui) huenda yakakosa kuwa sahihi, kamili au ya sasa kila wakati na pia inaweza kujumuisha kasoro za kiufundi na hitilafu za kimaandishi. Katika juhudi ya kuendelea kukupa maelezo kamili na sahihi kadri iwezekanavyo, kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria husika, maelezo yanaweza kubadilishwa au kusasishwa mara kwa mara bila ilani, ikijumuisha bila kipimo maelezo kuhusiana na sera, bidhaa na huduma zetu. Ipasavyo, unapaswa kuthibitisha maelezo yote kabla ya kuwasilisha na unawajibikia maamuzi yote kulingana na maelezo yalitopatianwa kupitia Huduma na hatutakuwa na dhima kwa ajili ya maamuzi hayo.

4.5 Upatikanaji. Ingawa tunajitahisi kukupa huduma bora zaidi, hatutoi hakikisho kwamba Huduma zitapatikana bila kudakizwa. Huenda Huduma zinakosa kupatikana kwa muda tu mara kwa mara kwa ajili ya udumishaji au sababu nyingine. Hatuwajibikii hitilafu, kutojumuishwa, kudakizwa, kufutwa, kasoro, kuchelewa katika operesheni au utumaji, kuharibika, kuibiwa au uharibifu kwenye mitambo ya mawasiliano au mawasiliano ya mtumiaji kufikiwa bila idhini au kuhitilafiwa. Hatuwajibikii matatizo yoyote au kuharibika kwa mtandao au mtambo wowote wa simu, mifumo ya mtandaoni ya kompyuta, vifaa vya kompyuta, programu, barua pepe kufeli kwa ajili ya matatizo ya kiufundi au msongamano wa watumiaji kwenye Intaneti au kwenye Huduma au zote pamoja, ikijumuisha majeraha kwa watumiaji au kwa mtu mwingine yeyote kuhusiana au kutokana na kushiriki au kupakua nyenzo kuhusiana na Huduma. Hatuwajibikii hasara au uharibifu wowote, hasara zozote za kifedha au faida zilizopotezwa, upotezaji biashara, au jeraha la kibinafsi au kifo, zinazotokana na matumizi ya mtu yeyote ya Huduma, Maudhui yoyote yaliyochapishwa kwenye au kupitia Huduma au kuwasilishwa na watumiaji, au utangamano wowote baina ya watumaiji wa Huduma, iwe ni mtandaoni au nje ya mtandao.

4.6 Mifumo Tanzu. Programu inayotumiwa kutengeneza WLD ni ya wazi na bila malipo kwa mtu yeyote anayetaka kuinakili na kuitumia. Hii inamaanisha kwamba mtu yeyote anaweza kutengeneza toleo lililobadilishwa la WLD, linaloitwa “Mfumo Tanzu.” Endapo kutakuwa na Mfumo Tanzu au ubadilishaji mwingine wowote wa mtandao wa Sarafu za Kidijitali, huenda hatutaweza kusaidia au kuunga mkono shughuli zozote zinazohusiana na Mfumo huo Tanzu. Miamala huenda ikakosa kukamilishwa, ikakamilishwa nusu, ikakamilishwa visivyo sahihi, au kucheleweshwa pakubwa wakati Mfumo Tanzu unapotokea. Hatuwajibikii hasara zozote zinazokukumba ambazo zinasababishwa kikamilifu au kwa sehemu tu na Mfumo Tanzu au mabadiliko mengine kwenye mtandao.

4.7 Huduma za Wahusika Wengine. Zinakopatikana (haswa tazama Sehemu ya 2.5), tunategemea watoa huduma wengine ili kukupa baadhi ya vipengele na utendaji ndani ya Programu hizi, kwa mfano uwezo wa kununua Sarafu za Kidijitali ukitumia sarafu za kawaida, au uwezo wa kubadilisha Mali fulani ya Kidijitali ili kupata nyingine. Hatutoi huduma hizi, na hatuhusiana na muamala wowote kama huo. Unategemea tu watoa huduma wengine ili kupata huduma hizi, na ni lazima uwe na akaunti za watoa huduma hawa wengine na ukubaliane na masharti yao. Hatuwezi

kukusaidia ukikumbwa na matatizo unapotumia huduma yao, na hatuwajibikii miamala yoyote unayofanya ukitumia watoa huduma wengine.

5. Mali Bunifu.

5.1 Umiliki. Programu yetu, programu ya kifaa tamba, Huduma, Maudhui na Alama (kama ilivyobainishwa hapa chini) na muundo, chaguo, na mpangilio wa Maudhui katika Huduma (“Mali Bunifu”) zinalindwa na hakimiliki, haki za alama za kibiashara, hataza, na haki nyingine za mali bunifu na sheria za Marekani na za nchi nyingine husika. Unakubali kuheshimu haki na sheria zote za mali bunifu, na pia ilani zozote au vikwazo vyovyote vya alama za kibiashara au hakimiliki vilivyo katika Makubaliano haya au Huduma. Hauwezi kuondoa ilani zozote za hakimiliki, alama za kibiashara, au hataza zilizo kwenye Mali Bunifu.

5.2 Alama za Kibiashara. Jina Tools for Humanity Corporation, nembo ya Programu ya World pamoja na nembo zote husiani, na kauli mbio ni alama za kibiashara au za huduma za Tools for Humanity Corporation au wanaoipea leseni (“Alama”). Hauwezi kunakili, kuiga, au kutumia Alama, zikiwa nzima au sehemu yake, bila kibali chetu kwa maandishi. Alama za kibiashara, majina, au nembo nyingine zote zilizotajwa kuhusiana na Huduma ni mali ya wamiliki wake halisi na hauwezi kunakili, kuiga, au kuzitumia, zikiwa nzima au sehemu yake, bila kibali kwa maandishi cha mmiliki wa alama husika ya kibiashara. Ujumuishaji wa alama zozote za wahusika wengine katika Huduma hakumaanishi kwamba tunawaunga mkono, au tunawapendekeza.

6. Leseni na Vikwazo

6.1 Leseni. Mradi iwe unastahiki kutumia Huduma na kulingana na uambatanaji wako na Sheria hizi, hapa tunakupa leseni yenye vipimo ya kufikia na kutumia Huduma.

6.2 Vikwazo vya Leseni. Hauwezi kuchapisha Maudhui kwenye tovuti yoyote ya Intaneti, Intraneti au Extraneti au kujumuisha maelezo katika hifadhidata au maktaba nyingine yoyote, na matumizi mengine yoyote ya maudhui yamepigwa marufuku kabisa. Matumizi yoyote ya Huduma kando na yaliyoidhinishwa hapa, bila idhini ya awali kwa maandishi, yamepigwa marufuku na yatasitisha leseni inayopatianwa hapa. Matuymizi hayo bila idhini pia yanaweza kukiuka sheria husika ikijumuisha bila kipimo sheria za hakimiliki an alama za kibiashara na kanuni na sheria husika za mawasiliano. Isipokuwa iwe imebainishwa moja kwa moja hapa, hakuna chochote kilicho katika Sheria hizi kitaonekana kama kinapeana leseni kwa haki za mali bunifu, iwe ni kwa kudai, kuashiria au vinginevyo. Tunaweza kubatilisha leseni hii wakati wowote bila ilani na kukiwa na bila sababu. kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria husika

6.3 Serikali. Ikiwa wewe ni mtumiaji wa Serikali ya Marekani, tunakupa leseni ya Huduma kama “Commercial Item” kama ambavyo neno hilo limefafanuliwa katika U.S. Code of Federal Regulations (tazama 48 C.F.R. § 2.101), na haki tunazokupa za Huduma ni sawa na haki tunazowapa wengine wote chini ya Sheria hizi.

7. Matumizi Yanayokubalika

7.1 Unaweza tu kutumia Huduma kwa matumizi yako ya kibinafsi pekee. Nyakati zote na kwa hiari yetu tunahifadhi haki ya kuhakiki, kughairi au kukatiza ufikiaji wako au matumizi yako ya Huduma kulingana na sheria husika. Vipengee kwenye orodha ya Matumizi Yalikatazwa ni mifano tu na orodha hii si kamilifu; huenda tukaongeza au kuondoa matumizi yaliyokatazwa kwa hiari yetu kulingana na sheria husika.

7.2 Matumizi Yaliyokatazwa yanajumuisha:

Shughuli Haramu: Shughuli yoyote ambayo inaweza kukiuka, au kusaidia katika ukiukaji wa, vikwazo vilivyowekwa na OFAC; kukiuka, au kusaidia katika ukiukaji wa, sheria zozote katika nchi ambako tunafanya biashara; kuhusisha faida kutokana na shughuli haramu; au kuchapisha, kusambaza, au kusambaza nyenzo zozote au maelezo yoyote haramu.

Matumizi Kupindukia au Udukuzi: Shughuli yoyote ambayo inaweka miundombinu yetu kazi nyingi kupindukia; inaathiri vibaya, kuhitilafiana, au kudhuru mfumo, data, au maelezo yoyote; inatuma au kupakia nyenzo zozote kwenye Huduma ambazo zina virusi, au programu nyingine zozote haribifu au za kufuta; au inajaribu kuingia bila idhini kwenye mifumo au mitandao ya kompyuta iliyounganishwa na huduma.

Matumizi Mabaya: Shughuli yoyote ambayo inahitilafiana na ufikiaji au matumizi ya Huduma ya mtu mwingine; inaharibia jina, kulaghai, kunyanyasa, kumtishia, au vinginevyo kukiuka haki za faragha, mali bunifu, au haki nyingine za kisheria za mtu mwingine; inachochea, kutishia, kuwezesha, kukuza, au kuhamasisha chuki, ubaguzi wa kimbari, au matendo ya uhalifu dhidi ya wengine; au

au inavuna, kutohoa, au kukusanya data za mtumiaji mwingine kutoka kwenye Huduma bila kibali.

Ulaghai na Matendo Mengine ya Biashara isiyo ya Haki: Shughuli yoyote ambayo inafanywa ili kutulaghai sisi, watumiaji wa wetu, au mtu mwingine yeyote; inatoa maelezo ya uwongo, yasiyo sahihi, au potovu kwetu; inaahidi faida kubwa zisizoeleweka au kuuza huduma bila manufaa kwa mnunuaji; au inaendeleza matendo mengine ya uwongo pamoja na michezo isiyo halali ya pata potea, mashindano, kamari, au michezo mingine ya bahati nasibu.

Ukiukaji Haki za Mali Bunifu: Shughuli yoyote ambayo inahusisha mauzo, usambazaji, au ufikiaji muziki, filamu, programu ghushi, au nyenzo nyingine zinazotumia leseni bila idhini mwafaka kutoka kwa wamiliki hakimiliki; inatumia mali bunifu (pamoja na Alama) bila idhini ya moja kwa moja au kwa njia ambayo inatudhuru sisi au biashara yetu; inaashiria kwa uwongo kwamba sisi tunaunga mkono au tunahusika; au inakiuka hakimiliki, alama ya kibiashara, haki ya kuwekwa hadharani au faraghani, au haki nyingine yoyote ya hakimiliki chini ya sheria.

8. Wahudumu wa Orb

Tunashirikiana na wakandarasi huru wa nchini wanaoitwa “Wahudumu wa Orb,” ambao wanawezesha shughuli ya kuwasajili watumiaji na kusaidia kujibu maswali ambayo huenda ukawa nayo kutuhusu sisi. Wahudumu hawa wa Orb wamepokea mafunzo na wanajua mengi kuhusu World Network. Hata hivyo, hatuna udhibiti wa na tunakanusha dhima yote inayotokana na wanachosema au jinsi wanavyoendesha shughuli zao. Wahudumu wa Orb si maajenti wala waajiriwa wetu kwa njia yoyote. Juhudi, mchakato, sera, kanuni, au jitihada zozote zinazochukuliwa na TFH kwa ajili ya maslahi ya watumiaji wake haiashirii uhusiano wa kiajira au kiajenti na Mhudumu wa Orb.

9. Uahirishaji

Huenda tukasimamisha na kuzuia ufikiaji wako wa Huduma: (i) Tunahitajika kufanya hivyo chini ya amri halali, amri ya mahakama, au amri ya kimkataba ya mamlaka ya serikali; (ii) Tuna sababu ya kutuhumia kwamba unatumia Huduma kwa Matumizi Yaliyokatazwa; (iii) Matumizi yako ya Huduma yanaathiriwa na kesi, uchunguzi au mchakato unaoendelea wa serikali na/au tunaona shughuli zako zinahusisha hatari kubwa ya kisheria au kutoambatana na kanuni za kiudhibiti; (iv) Wabia wetu wa huduma hawawezi kuendeleza matumizi yako; (v) Unachukua hatua yoyote ambayo tunaona kwamba inaepuka vidhibiti vyetu (kama vile na sio tu kujaribu kutengeneza akaunti nyingi)..

10. Si Utoaji Ofa ya Faida za Hisa au Bidhaa

Maudhui ya Huduma hayajumuishi ofa ya kununua au kuuza au ushawishi wa ofa ya kununu au kuuza uwekezaji, hisa, nia za ubia, bidhaa au vipengee vingine vyovyote vya kifedha; maudhui au Huduma pia hazijumuishi, na haziwezi kutumika katika, au kuhusiana na, ofa au ushawishi wa mtu yeyote katika jimbo au mamlaka yoyote ambako ofa au ushawishi huo haujaidhinishwa au hairuhusiwi, au kwa mtu yeyote kwa ambaye ni kinyume cha sheria kumpa ofa au ushawishi huo.

11. Maudhui

11.1 Kutegemea Maudhui; Mabadiliko kwenye Huduma. Maelezo na nyenzo tunazokupa kupitia Huduma (“Maudhui”) ni za kimaelezo pekee, na hatutoi hakikisho kuhusiana na usahihi, umuhimu, au ukamilifu wake, kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria husika. Unapotegemea Maudhui yetu unafanya hivyo kwa shauri yako. Hatuna dhima wala wajibu kwa hatua zozote unazochukua au kutochukua kwa sababu ya maudhui, au kwa mtu yeyote unayemtumia Maudhui. Kauli za watumiaji wengine wakielezea jinsi wanavyotumia Huduma zilizo kwenye Huduma au mahali kwingineko hazipaswi kuchukuliwa kama tunaunga mkono kauli zao ikiwa kauli hizo haziendanishi na Sheria hizi au Maudhui yetu. Tunaweza kusasisha Maudhui mara kwa mara, lakini Maudhui hayo huenda yakakosa kuwa kamilifu au iliyosasishwa, hatuna jukumu kwako la kusasisha Maudhui au sehemu nyingine yoyote ya Huduma. Tunaweza kubadilisha au kusitisha, kwa muda tu au kabisa, Maudhui au Huduma zote au sehemu yoyote yake bila ilani ya awali kwako, kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria husika. Hatutakuwa na dhima kwa mabadiliko, uahirishaji, au usitishaji wowote wa Maudhui au Huduma zote au sehemu yake, kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria husika..

11.2 Huduma na Maudhui ya Wahusika Wengine. Tunaweza kupatiana viungo elekezi vya nyenzo za kielimu, webinar, mikutano, na promosheni kwenye mitandao ya kijamii (Huduma za “Wahusika Wengine”) ambayo inawezesha kushiriki na ushirikiano miongoni mwa watumiaji wetu na wahusika wengine. Ukishiriki maelezo yoyote ya kibinafsi, picha, maoni, maudhui, au data nyingine zozote kwenye huduma hizo, unafanya hivyo kwa shauri yako, na matumizi yako ya huduma hizo upo chini ya sheria za matumizi na sera za faragha za huduma hizo, na sio zetu. Unapaswa kupitia sheria za matumizi za kila Huduma ya Mhusika Mwingine ili kuelewa vyema haki zako, na jinsi ambavyo majukwaa hayo yanavyotumia data zako. Hatuwajibikii hasara, udukuzi, au matumizi yoyote mabaya ya data zako vyovyote vile kuhusiana na Huduma yoyote ya Mhusika Mwingine (pamoja na

utelekezaji) isipokuwa iwe dhima hiyo haiwezi kuzuiliwa chini ya sheria husika. Matumizi yako ya maelezo yoyote yanayotolewa na Huduma ya Mhusika Mwingine (“Maudhui ya Wahusika Wengine”) ni kwa shauri yako, na hatukupi ahadi zozote kwamba Maudhui ya Wahusika Wengine ni sahihi, kamilifu, halali, au mwafaka kwa hali yako binafsi. Maudhui ya Wahusika Wengine yanajumuisha maelezo yaliyotolewa na watumiaji wengine na hatujayaunga mkono.

11.3 Maudhui ya Mtumiaji. Kama memba wa jamii wa Worldcoin, huenda ukachapisha ujumbe, data, programu, picha, video, au maudhui mengine (“Maudhui ya Mtumiaji”) kwenye ubao wa ujumbe, blogi, akaunti za mitandao ya kijamii inayomilikiwa nasi, pamoja na maeneo mengine yanayopatikana hadharani kwenye Huduma. Majukwaa haya huenda ni sisi tunayandaa au kuandaliwa na Mtoa Huduma Mwingine kwa niaba yetu. Unawajibikia Maudhui yote ya Mtumiaji ambayo unawasilisha, kupakia, kuchapisha, au kuhifadhi kupitia Huduma. Ni lazima uto maonyo, maelezo, na ufichuaji wote unaohitajika na mwafaka kuhusiana na Maudhui yako ya Mtumiaji. Hatuwajibikii Maudhui yote ya Mtumiaji ambayo unawasilisha kupitia Huduma.

11.4 Leseni ya Maudhui ya Mtumiaji. Kwa kuwasilisha Maudhui ya Mtumiaji kwetu, unawakilisha kwamba una haki zote zinazohitajika kwenye Maudhui hayo ya Mtumiaji na kwa hivyo kutupatia leseni ya milele, ya kote ulimwenguni, isiyo ya kipekee, bila hakimiliki, inayoweza kutolewa leseni ndogo, na inayoweza kuhamishika ya kutumia, kusambaza, kuandaa kazi tohozi, kubadilisha, kuonyeshana, na kutekeleza maudhui yote ya Mtumiaji au sehemu yake katika uuzaji na promosheni zetu, na malengo mengine halali ya kibiashara yanayohusiana na Huduma. Tunaweza kusambaza tena kazi tohozi za Maudhui yako ya Mtumiaji kwa mfumo wowote na kupitia vyombo vyovyote vya habari tunavyochagua. Hapa pia unatupatia sisi na watumiaji wengine leseni isiyo ya kipekee ya kutumia, kufikia, kuzalisha tena, kusambaza, kubadilisha, na kuonyeshana, na kutekeleza Maudhui yako ya Mtumiaji kupitia Huduma. Sehemu ya 11.4 itatumika kwa kiwango kamilifu kinachoruhusiwa na sheria husika.

11.5 Vikwazo vya Maudhui ya Mtumiaji. Unakubali kutotumia, kutoruhusu mhusika mwingine yeyote kutumia, Huduma kuchapisha au kutuma Maudhui yoyote ya Mtumiaji ambayo: (a) yanaharibiana jina au sifa, au kufichua masuala ya faraghani na ya kibinafsi kumhusu mtu yeyote; (b) ni chafu, ya uchi, ya kunyanyasa, ya kutishia, ya chuki, ya kuudhi kwa misingi ya mbari au kabila; ya kuhamasisha tabia ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa hatia ya kijinai, inaweza kupelekea dhima ya umma, au ya kukiuka sheria yoyote, au vinginevyo haifai; (c) inaweza kukiuka haki za mali bunifu za wengine, pamoja na maandishi, ujumbe au programu, siri za kibiashara zenye hakimiliki au maelezo mengine ya hakimiliki, au alama za kibiashara au huduma zinazotumika kwa njia inayokiuka; au (d) inayohitilafiana na matumizi ya Huduma na watumiaji wengine. Unawakilisha kwetu kwamba unachapisha Maudhui ya Mtumiaji kwenye Huduma kwa hiari; kwa kuchapisha Maudhui ya Mtumiaji hakuleti uhusiano wa Mwajiri na mwajiriwa baina yako nasi. Hauwezi kunakili wala kutumia anwani za barua pepe, nambari za simu, salio, majina ya mtumiaji, au maelezo nyingine ya kibinafsi kuhusu watumiaji wengine bila kibali chao. Barua pepe, barua, simu, au mawasiliano mengine bila maana kwa watumiaji wengine kupitia Huduma au kwa mbinu nyingine yoyote kumepigwa marufuku.

11.6 Malalamishi na Maudhui Kuondolewa kwa Ajili ya DMCA. Ikiwa unaamini kwamba alama yako ya kibiashara au kazi yenye hakimiliki imekiukwa na Maudhui yetu au Maudhui ya Mtumiaji kwenye Huduma au vinginevyo inachapishwa kwa njia ambayo inaashiriwa kwamba inaunga mkono au inahusiana nasi, tafadhali tutumie barua pepe kwa anwani [email protected] ikiwa na mada ya “[Trademark/Copyright] Complaint,” bila kujali tukio husika. Ili lalamishi lako liwe fanisi na ili sisi tuweze kuchukua hatua chini ya Sheria ya Hakimiliki ya Milenia ya Kidijitali (Digital Millennium Copyright Actm, “DMCA”), ni lazima ufuate mahitaji ya DMCA kwa kujumuisha maelezo yafuatayo katika barua pepe yako:

  • Utambuaji wazi wa kazi au alama iliyo na hakimiliki ambayo unadai imekiukwa, pamoja na nambari ya Usajili wa Hakimiliki ikiwa kazi hiyo imesajiliwa;
  • Utambulisho wa kazi au alama ambayounadai imekiukwa na ambayo ungependa iondolewe;
  • Kiungo elekezi au mwelekeo mwingine wazi wa kutuiwezesha kupata maudhui ambayo yanakiuka;
  • Anwani yako ya barua pepe, anwani ya barua, na nambari ya simu; na
  • Kauli iliyotiwa sahihi kwamba una imani kwa nia nzuri kwamba maudhui yanakiuka, kwamba maelezo unayotoa ni sahihi, na kwamba wewe ndiye mmiliki au umeidhinishwa kumwakilisha mmiliki wa maudhui hayo.

Pia unapaswa kuelewa kwamba chini ya Sehemu ya 512(f) ya DMCA, mtu yeyote ambaye anatuma ilani za uwongo za ukiukaji huenda akawa na dhima kwa hasara, kwa hivyo tafadhali usifanye madai ya uwongo. Tunaweza kushiriki maelezo au mawasiliano yoyote unatupatia uliyofanya na wahusika wengine, pamoja na mtu aliyepakia kwenye Huduma nyenzo zinazodaiwa kukiuka.

Tunapopokea ilani ya kweli ya ukiukaji, sera yetu ni: (a) kuondoa mara moja au kulemaza ufikiaji wa maudhui yanayokiuka; (b) kumwarifu mtu aliyepakia maudhui yanayokiuka kwamba tumeondoa au tumelemaza ufikiaji wa maudhui hayo; na (c) kwa wanaorudia

hatia, kusitisha uwezo wao wa kufikia Huduma. Tukipokea ilani ya kukataa kutoka kwa mtu huyo, tunaweza kukutumia nakala ya ilani hiyo ya kukataa ili kuelezea kwamba huenda tukarejesha maudhui yaliyoondolewa au tukaacha kuyalemaza ndani ya siku 10 za biashara. Isipokuwa uwasilishe kesi ukitaka amri ya mahakama dhidi yetu au dhidi ya mtu ambaye alipakia maudhui hayo, tutarejesha ufikiaji wa maudhui yaliyoondolewa ndani ya siku 10 hadi 14 za biashara au nyingi zaidi baada ya kupokea ilani ya kukataa, kwa hiari yetu.

12. KANUSHO LA HAKIKISHO

12.1 Matumizi yako ya Huduma ni kwa shauri yako. Huduma, WLD, maudhui na mali bunifu nyingine zote zinatolewa “KAMA ZILIVYO” na “KAMA ZINAVYOPATIKANA” bila uwakilisho au hakikisho lolote, iwe ni moja kwa moja, imeashiriwa, au chini ya sheria. Kwa kiwango kamili kinachoruhusiwa na sheria husika, tunakanusha hakikisho zozozote zilizoashiriwa za umiliki, kibiashara, uzima kwa ajili ya dhumuni fulani, au kutokiuka kuhusiana na vipengele, maudhui, au Mali Bunifu nyingine iliyo katika Huduma. Baadhi ya maeneo ya mamlaka hayaruhusu kutojumuishwa kwa hakikisho zilizoashiriwa, kwa hivyo kutojumuishwa huku huenda kukakosa kukuathiri. Hatuungami, kuhakikishia, au kuwajibikia matangazo, ofa, au kauli zozote zinazotolewa na wahusika wengine, pamoja na watumiaji wengine kuhusiana na Huduma.

12.2 Hatutoi uwakilisho au hakikisho zozote kwamba (a) ufikiaji wa Huduma zote au sehemu yake utakuwa endelevu, bila kudakizwa, kwa wakati, salama, au bila hitilafu; (b) kwamba Huduma au maudhui ni sahihi, kamilifu, aminifu, au ya sasa; (c) kwamba Huduma hazina virusi au vipengele vingine haribifu; au (d) kwamba Huduma au maudhui yatatimiza mahitaji, au matarajio yako.

12.3 Aidha, hatutoi uwakilisho au hakikisho zozote kuhusiana na uhalali wa Huduma au WLD kwa matumizi yoyote, au kwamba Huduma au WLD zitatimiza mahitaji yoyote ya kiudhibiti au uambatanaji. Una wajibu wa kubainisha na kuambatana na vikwazo na mahitaji yote ya kisheria na kiudhibiti ambayo yanatawala matumizi yako ya Huduma au WLD. Isipokuwa kwa kauli za moja kwa moja zilizobainishwa katika Sheria hizi, hapa unakiri na kukubaliana kwamba haujategemea kauli nyingine yoyote au uelewa mwingine wowote, iwe ni kwa maandishi au matamshi, kuhusiana na ufikiaji na matumizi yako ya Huduma au WLD.

12.4 Hatutendi na hatuwezi kutenda kama mshauri wako kuhusiana na masuala yoyote au kifedha, kisheria, uwekezaji, na ushuru. Maudhui yoyote ni sahihi kuanzia tarehe iliyoonyeshwa. Mipango, makadirio, utabiri, malengo na/au maoni yoyote yaliyotolewa hapa yanakabiliwa na hatari, kutokuwa na uhakika na dhana, na kwa hivyo yanaweza kuwa si sahihi na yanaweza kubadilika bila ilani. Hakuna maudhui yanapaswa kutegemewa.

Baadhi ya maelezo yanayopatikana hapa yanaweza kuwa yamechukuliwa kutoka kwa wahusika wengine. Ijapokuwa vyanzo kama hivyo vinachukuliwa kuwa vya kuaminika, hatujathibitisha moja kwa moja maelezo hayo yote na hatutoi uwakilisho kuhusiana na usahihi wake. Hatujasajiliwa kama wauzaji hisa au washauri wa uwekezaji. Hatutoi uwakilisho, na haswa tunajitenga nahakikisho zote, za moja kwa moja, zilizoashiriwa, au za kisheria, kuhusiana na usahihi, wakati, au ukamilifu wa nyenzo zozote zilizo kwenye Huduma. Maudhui yetu yaliyotolewa ni ya kimaelezo jumla, na una wajibu wa kubaini kana kwamba utatumia Huduma au la. Unatambua kwamba kufanya biashara, kutumia, na kumiliki Sarafu za Kidijitali kuna hatari kubwa. Unaweza ukapoteza fedha zote zilizo kwenye pochi lako. Unatambua kwamba Huduma inaweza kuwa chini ya vikwazo vya uuzaji nje ya nchi na vikwazo vya kiuchumi vinavyowekwa na sheria ya Marekani.

12.5 Hatuna dhima kwako au kwa mhusika mwingine kwa ajili ya marekebisho yoyote au usitishaji wa Huduma, au uahirishaji au usitishaji wa ufikiaji wako wa Huduma.

13. KIPIMO CHA DHIMA

13.1 Hatutengi wala kuwekea kipimo dhima yetu kwako ambapo ni kinyume cha sheria kufanya hivyo. Katika nchi ambako aina za mambo yasiyojumuishwa zilizo hapa chini ambazo haziruhusiwi, tuna wajibu kwako tu kwa hasara na uharibifu ambao haungeweza kutabirika kutokana na sisi kutokuwa waangalifu na kutotumia ujuzi tosha au sisi kukiuka mkataba wetu nawe. Aya hii haiathiri haki za mtumiaji ambazo haziwezi kuondolewa au kuwekewa kipimo na mkataba au makubaliano yoyote.

13.2 Kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria, unakubaliana kwamba hakuna wakati sisi au maafisa, wakurugenzi, waajiriwa, wakandarasi, maajenti, washirika wetu, au kampuni zetu tanzu (“Wahusika wa TFH”) tutakuwa na dhima kwako kwa ajili ya hasara zozote zisizo za moja kwa moja, za kiadhabu, za bahati mbaya, maalum, zinazotokana na jambo lingine, au za kuigwa, pamoja na hasara za kupoteza faida, nia nzuri, matumizi, data, au mali nyingine isiyoweza kugusika, iwe dhima hiyo imewekwa kwa msingi wa ukiukaji au vinginevyo, au iwe Wahusika wa TFH wamefahamishwa au hawajafahamishwa kuhusu uwezekano wa hasara hizo zinazohusiana au kutokana na: (a) matumizi yako au wewe kutoweza kutumia Huduma, Sarafu zako za Kidijitali, au World Network; (b) kutoweza kufikia ua kusitishwa kwa Huduma; (c) udukuzi, hitilafu, ufikiaji bila idhini au ubadilishaji wa muamala wowote au Data zako; (d) muamala au makubaliano yoyote yanayofanyika baina yako na mhusika mwingine kupitia Huduma; (e) shughuli au mawasiliano yoyote na wahusika wengine; (f) matendo ya Wahudumu wa Orb, (g) upotezaji wowote wa thamani ya Sarafu zozote

za Kidijitali; (h) Maudhui yoyote ya Wahusika Wengine yanayofikiwa kwenye au kupitia Huduma; (i) hitilafu, makosa, au kasoro kwenye Maudhui yetu; (j) majeraha ya kibinafsi au uharibifu wa mali wa aina yoyote ile unaotokana na ufikiaji wowote na matumizi ya Huduma; (k) virusi, au virusi vinavyoweza kutumwa kwenye au kupitia Huduma; au (l) tabia ya kuharibia jina, inayodhuru, au haramu ya mhusika mwingine yeyote. Kipimo hiki cha dhima kitatumika ikiwa hasara zinaibuka kutoka na matumizi au matumizi mabaya ya, au kwa ajili ya kutegemea TFH au Huduma, bila kujali kutofaulu kwa lengo muhimu la suluhu yoyote na kwa kiwango kamili kinachoruhusiwa na sheria husika.

13.3 Hakuna wakati ambapo Wahusika wa TFH watakuwa na dhima kwako kwa ajili ya madai, kesi, dhima majukumu, uharibifu, hasara, au gharama zozote za moja kwa moja kwa kiwango kinachozidi $100.00. Ikiwa haujaridhika na Huduma, unakubaliana kwamba suluhu yako pekee itakuwa ya wewe kuacha kutumia Huduma. Kipimo hiki cha dhima kitatumika kwa kiwango kamili kinachoruhusiwa na sheria husika.

13.4 Kibali na Uondoaji Lawama. Unakubali kutetea, kuondolea lawama, na kuchukulia Wahusika wa TFH kuwa wasiodhuru dhidi ya madai, hasara, gharama, dhima, na ada za wakili zinazoletwa dhidi ya Mhusika wa TFH na mhusika yeyote mwingine kuhusiana na kutokana na: (a) matumizi yako ya Huduma; (b) ukiukaji wako wa Sheria hizi; (c) ukiukaji wako wa haki za mtu mwingine; (d) tabia yako kuhusiana na Huduma; au (e) matumizi yako ya WLD, Sarafu zozote za Kidijitali, au mtandao wa Worldcoin. Baadhi ya mamlaka zinawekea kipimo kiwango cha uondoaji lawama wa watumiaji, kwa hivyo baadhi ya vipengele au vipengele vyote katika aya hii huenda visikuathiri. Ikiwa una jukumu la kumwondolea lawama Mhusika yeyote wa TFH, tunahifadhi haki, kwa hiari yetu binafsi, ya kudhibiti hatua au kesi yoyote na kubaini kana kwamba tutafidiana na kwa masharti gani.

IKIWA WEWE NI MKAAZI WA CALIFORNIA, unaondoa haki zako za kupata manufaa na kinga za sheria ya California Civil Code § 1542, ambayo inajumuisha: “[a] kibali jumla hakitumiki kwa madai kwamba mtoa kibali hajui au hadhanii kuwa angenufaika wakati alipokuwa akiidhinisha kibali na kwamba, ikiwa alikuwa anajua, ingeathiri pakubwa kiwango cha fidia kutoka kwa anayepokea kibali.”

14. Sheria Inayotawala

Sheria za Jimbo la Carlifonia zitatumika kwenye Makubaliano haya na migogoro yoyote inayoibuka kutokana au kuhusiana na Makubaliano haya. Sheria inayotawala iliyotajwa katika sehemu hii itatumika bila kujali ukinzani wa sheria. Unakubali zaidi kwamba Huduma itachukuliwa kuwa ya Jimbo la California pekee, na kwamba ingawa Huduma zinaweza kupatikana katika maeneo mengine ya mamlaka, upatikanaji wake hauibui mamlaka ya kijumla au kibinafsi katika jukwaa lolote nje ya Jimbo la California.

15. USULUHISHAJI MIGOGORO, MCHAKATO WA USULUHISHAJI NA UONDOAJI KESI YA KUNDI

15.1 TAFADHALI SOMA AYA ZIFUATAZO KWA MAKINI. ZINAKUHITAJI WEWE KUSULUHISHA MIGOGORO NASI KUPITIA MCHAKATO WA USULUHISHAJI BINAFSI MBELE YA MSULUHISHAJI MMOJA, NA SIO KAMA MMOJA YA WANAOLETA KESI YA KUNDI. MCHAKATO WA USULUHISHAJI UNAKUZUIA KUTOTUSHTAKI MAHAKAMANI AU KUTOKUWA NA KESI MBELE YA HAKIMU, INGAWA UNAWEZA KULETA MGOGORO DHIDI YETU KATIKA MAHAKAMA YA MADAI MADOGO IKIWA UNASTAHIKI.

15.2 Tutatumia jitihada zetu bora kusuluhisha migogoro yoyote inayoweza kutokea kupitia majadiliano yasiyo rasmi ya nia nzuri. Endapo mgogoro utaibuka, ni lazima uwasiliane nasi kwa kututumia barua pepe kwa anwani [email protected] ili tuweze kujaribu kuusuluhisha bila kutumia mchakato rasmi wa usuluhishaji migogoro. Ikiwa hatutaweza kufikia suluhu kwa njia isiyo rasmi ndani ya siku 60 za kutumiana barua pepe, na uchague kuibua dai kulingana na sheria ya shirikisho au jimbo, sheria ya kawaida, kulingana na mkataba, ukiukaji, ulaghai, maelezo potovu au msingi mwingine wowote wa kisheria, au kesi nyingine yoyote rasmi inayohusiana au kutokana na Sheria hizi, Maudhui au Huduma (kila moja, “Mgogoro”), kisha ukubali kusuluhisha Mgogoro huo kupitia mchakato wa usuluhishaji unaokufunga, kwa msingi wa mtu binafsi kulingana na masharti yafuatayo (kwa pamoja, “Makubaliano ya Mchakato wa Usuluhishaji”):

Mchakato wa usuluhishaji utaendeshwa faraghani na msuluhishaji mmoja. Msuluhishaji atatumia vipengele vya kipimo na sheria nyingine zote husika kuu na ataheshimu haki ya kutofichua maelezo fulani yanayotambuliwa na sheria husika.

Mgogoro utasuluhishwa kikamilifu na mchakato wa usuluhishaji unaoendeshwa na JAMS kulingana na Sheria za Usuluhishaji Rahisi za JAMS (JAMS Streamlined Arbitration Rules), isipokuwa iwe kiwango kilichokadiriwa cha Mgogoro ni $250,000 au zaidi, ambapo Sheria za Usuluhishaji Mgumu za JAMS (JAMS Comprehensive Arbitration Rules) zitatumika. Mchakato wa usuluhishaji utafanyika mjini San Francisco, California, isipokuwa wewe na sisi tukubaliane kuufanyia kwingineko. Unakubali kwamba mahakama za serikali ya kitaifa na jimbo mjini San Francisco, California ndiko mahali kunakofaa kwa kesi zozote za rufaa za tuzo la mchakato wa usuluhishaji au kwa kesi za mahakamani endapo kifungu hiki cha mchakato wa usuluhishaji katika Makubaliano haya kinapatikana kuwa hakiwezi kutekelezeka.

Katika mchakato wowote wa usuluhishaji, bila kujali eneo lake, wahusika hawataomba kufahamishwa awali kuhusu ushahidi wa mhusika yule mwingine, naye msuluhishaji hatawaruhusu wahusika kuhusika katika kufahamishana awali kuhusu ushahidi wa kila upande; badala yake, kila mhusika atafichua ushahidi wake katika saa na tarehe itayokubalianwa kabla ya kipindi cha mwisho cha mchakato wa usuluhishaji.

Makubaliano haya ya Usuluhishaji yanasimamia uwezo wa kutekelezeka, uwezo wa kubatilishwa, wigo, na uhalali wa Makubaliano ya Mchakato wa Usuluhishaji au sehemu yoyote ya Makubaliano ya Mchakato wa Usuluhishaji, na Migogoro mingine yote inayoibuka kuhusiana au kutokana na ufafanuzi au matumizi ya Makubaliano ya Mchakato wa Usuluhishaji; na masuala hayo yote yataamuliwa na msuluhishaji na sio mahakama wala hakimu.

Ikiwa msuluhishaji au msimamizi wa mchakato wa usuluhishaji atakutoza ada za kuandikisha madai au gharama nyingine za ofisi, tutakufidia, baada ya ombi, kwa kiwango ambacho ada au gharama hizo hazitazidi zile ambazo ungelipia ikiwa ingekuwa kesi mahakamani. Pia tutalipia ada na gharama za ziada ikiwa inaagizwa na sheria za msuluhishaji au sheria husika.

Kwa ombi la mhusika yeyote, mchakato wote wa usuluhishaji utafanywa kwa usiri mkubwa na, hivyo basi, hati zote, ushahidi wote, na rekodi zote zitapokewa, kusikizwa, na kuhifadhiwa na msuluhishaji kwa siri na kufungiwa, na kuweza kufikiwa na wahusika pekee, mawakili wao husika, na wataalam wao husika, washauri, au mashahidi ambao wamekubali, hapo awali na kwa maandishi, kupokea maelezo hayo yote kama siri ili kutumiwa kwa malengo pekee ya mchakato wa usuluhishaji.

Kando na kesi za kundi na suluhu zilizojadiliwa katika Makubaliano haya ya Mchakato wa Usuluhishaji, msuluhishaji ana mamlaka ya kutoa suluhu yoyote ambayo vinginevyo ingepatikana mahakamani.

Uamuzi wowote wa fidia inayotuzwa na msuluhishaji unaweza kukubalika katika mahakama yoyote yenye mamlaka adilifu.

Ikiwa hitaji la kufanya Mchakato wa Usuluhishaji au kukataliwa kwa kesi za kundi na Migogoro mingine iliyoletwa kwa niaba ya wahusika wengine walio katika Makubaliano haya ya Mchakato wa Usuluhishaji litapatikana kuwa haliwezi kutekelezeka, basi ni vipengele pekee ambavyo haviwezi kutekelezeka vitakavyochukuliwa kuwa vimeondolewa kutoka kwenye Sheria hizi na majukumu yote yanayosalia katika Sheria hizi yataendelea kutekelezwa kikamilifu.

15.3 Haki ya Kujiondoa ya Siku 30. Una haki ya kujiondoa na kutofungwa na Makubaliano haya ya Mchakato wa Usuluhishaji kwa kutuma barua pepe kwa [email protected] kutoka kwa anwani ya barua pepe ambayo ulitumia kusajili programu yako na ikiwa na Mada ya: “ARBITRATION AND CLASS ACTION WAIVER OPT-OUT. Ni lazima utume barua pepe yako ndani ya siku 30 baada ya kukubaliana na Sheria hizi, kando na hivyo utalazimika kutumia mchakato wa usuluhishaji ili kusuluhisha Migogoro kulingana na masharti ya Makubaliano haya ya Mchakato wa Usuluhishaji. Ukijiondoa kwenye Makubaliano haya ya Mchakato wa Usuluhishaji, sisi pia haitafungwa na Makubaliano ya Mchakato wa Usuluhishaji.

15.4 Mabadiliko kwenye Makubaliano haya ya Mchakato wa Usuluhishaji. Tutakupa ilani ya siku 30 ya mabadiliko yoyote kwenye sehemu ya Sheria hizi iliyo na kichwa “Usuluhishaji Migogoro, Mchakato wa Usuluhishaji na Uondoaji Kesi ya Kundi” kwa kukupatia ilani, na mabadiliko hayo yataanza kutumika siku 30 baada ya kupokea ilani kutoka kwetu. Mabadiliko kwenye sehemu ya Usuluhishaji Migogoro, Mchakato wa Usuluhishaji na Uondoaji Kesi ya Kundi yatatumika tu kwa Migogoro inayoibuka baada ya siku ya 30. Ikiwa mahakama au msuluhishaji ataamua kwamba mabadiliko kwenye sehemu hii hayawezi kutekelezwa au si halali, basi mabadiliko hayo yataondolewa kwenye Sheria hizi nayo mahakama au msuluhishaji atatumia masharti ya toleo la kwanza la Makubaliano ya Mchakato wa Usuluhishaji yaliyoanza kutumika baada ya kuanza kutumia Huduma. Unaweza kutumia haki yako ya kujiondoa kwenye masharti mapya ya Makubaliano ya Mchakato wa Usuluhishaji kwa kufuta utaratibu uliobainishwa katika sehemu iliyo hapa juu kwa kichwa “Haki ya Kujiondoa ya Siku 30.”

Makubaliano haya ya Mchakato wa Usuluhishaji yataendelea kutumika hata Sheria hizi zikisitishwa, na wewe kuacha kutumia Huduma.

Bila kujali chochote kilicho katika Makubaliano haya ya Mchakato wa Usuluhishaji, mhusika yeyote anaweza kuanzisha kesi ya kumwondolea wajibu ili kusitisha matumizi bila idhini au matumizi mabaya ya Huduma, au ukiukaji wa haki za mali bunifu (kwa mfano, alama za kibiashara, siri za kibiashara,

hakimiliki, au haki za hataza) bila kwanza kuhusisha mchakato wa usuluhishaji au mchakato usio rasmi wa kusuluhisha migogoro ulioelezewa hapa juu.

16. Misimamo Jumla

16.1 Hakuna Kuondoa Haki; Ubaya; Kutoweza Kupewa Jukumu. Sisi kushindwa kutekeleza kipengele si kuondoa haki yetu ya kufanya hivyo baadaye. Ikiwa kipengele fulani kitapatikana kuwa hakiwezi kutekelezeka, vipengele vinavyosalia vya Sheria hizi vitasalia kutumika kikamilifu na kipengele kinachoweza kutekelezeka kitachukua nafasi hiyo ili kuonyesha jitihada zetu kadri iwezekanavyo, kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria husika. Hauwezi kupeana haki zako zozote chini ya Sheria hizi, na jaribio lolote la kufanya hivyo litakuwa bure. Tunaweza kupeana haki zake kwa mshirika wake yeyote au kampuni yoyote yake tanzu, au kwa mrithi yeyote kwa ajili ya shughuli yoyote inayohusiana na Huduma.

16.2 Makubaliano Kamili. Makubaliano haya yanajumuisha makubaliano yote na kamili baina yako nasi kuhusiana na Huduma na yana nguvu kuliko maelewano, makubaliano, uwakilisho, na hakikisho zote za hapo awali, kwa maandishi na matamshi, kuhusiana na Huduma. Vichwa vya sehemu mbalimbali katika Sheria hizi ni vya kurahisisha mambo tu na havitatawala maana au ufafanuzi wa kipengele chochote.

16.3 Kudumu. Vipengele vyote vya Sheria hizi kuhusiana na uahirishaji au usitishaji, madeni kwa TFH, matumizi jumla ya Huduma, Migogoro na TFH, na pia vipengele ambavyo vinazidi wakati wa usitishaji wa Sheria hizi, vitadumu hata baada ya usitishaji wa Sheria hizi.

16.4 Uhusiano wa Wahusika. Hakuna kitu chochote katika Sheria hizi kitachukuliwa au kinakusudiwa kuchukuliwa, wala kitakachokufanya na TFH kuchukuliwa kuwa wabia, wanabiashara wenza, au vinginevyo kama washirika wa pamoja katika faida, na wewe wala TFH hamtachukuliwa kuwa ajenti wa yule mwingine. Hii inajumuisha kwamba hakuna kitu chochote katika Sheria hizi kinaweka au kinakusudiwa kuweka uhusiano wowote wa ajira baina yako na TFH.

16.5 Hakuna Majukumu ya Ushauri wa Kitaalamu au Kifedha. Maudhui yote yanayotolewa nasi ni ya malengo ya kimaelezo pekee na hayapaswi kuchukuliwa kama ushauri wa kitaalamu. Haupaswi kuchukua, au kutochukua, hatua yoyote kwa sababu ya maelezo yaliyo katika Sheria hizi. Kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya kifedha, kisheria, au mengine yanayohusiana na Huduma au Sarafu zozote za Kidijitali, unapaswa kutafuta ushauri huru wa kitaalamu kutoka kwa mtu ambaye ana leseni na amehitimu katika nyanja ambayo ushauri huo unafaa. Sheria hizi hazikusudiwi, na hatengenezi wala kutuwekea majukumu yoyote ya kifedha. Kwa kiwango kamili kinachoruhusiwa na Sheria, unakiri na kukubali kwamba hatuna majukumu au dhima za kifedha kwako au kwa mhusika mwingine yeyote, na kwamba kwa kiwango ambazo majukumu au dhima hizo huenda zikakuwepo kisheria, majukumu au dhima hizo zimekanushwa, kuondolewa, na kutupiliwa mbali jinsi isiyoweza kubatilishika. Aidha unakubali kwamba wajibu na majukumu pekee ambayo tuko nayo kwako ni yale ambayo yamebainishwa moja kwa moja katika Sheria hizi.

16.6 Mabadiliko kwenye Udhibiti. Endapo tutanunuliwa au kuungana na shirika lingine, au vinginevyo kupeana majukumu mengine kwa shirika husika au linalorithi au shirika lingine ambalo tutaona ni kwa maslahi bora ya Watumiaji, basi tunahifadhi haki, katika tukio lolote kati ya matukio haya, ya kuhamisha au kupatiana Data ambazo tumekusanya kutoka kwako kama sehemu ya muungano huo, kunukuliwa huko, uuzaji huo, au badiliko nyingine kwenye udhibiti, kulingana na sheria husika.

16.7 Mambo Yasiyotarajiwa na Yasiyoweza Kudhibitiwa. Hatutawajibikia kuchelewa, utendakazi duni, au huduma kudakizwa ambao moja kwa moja au vinginevyo kunapelekea mabadiliko makubwa sokoni katika thamani ya Sarafu za Kidijitali, tendo lolote la Mungu, matendo ya mamlaka za kijamii au kijeshi, matendo ya magaidi, usumbufu wa umma, vita, mgomo, dharura ya afya, mgogoro wa leba, moto, mawasiliano ya simu au huduma za Intaneti na huduma za mtandao kudakizwa, vifaa au programu kutofanya kazi, au jambo au hali yoyote ambayo haiwezi kudhibitiwa (kila moja, “Tukio la Mambo Yasiyotarajiwa na Yasiyoweza Kudhibitiwa”). Utokeaji wa Tukio la Mambo Yasiyotarajiwa na Yasiyoweza Kudhibitiwa hautaathiri uhalali na uwezo wa kutekelezeka wa kipengele chochote kilichosalia cha Sheria hizi.

16.8 Maduka ya Programu. Mahali ambapo unapakua Programu zetu kutoka kwa duka lolote la programu au jukwaa la usambazaji kando na Apple App Store, ikijumuisha Google Play Store ("Jukwaa la Usambazaji") unakubali kwamba:

Sheria hizi ni kati yako nasi, na sio na mtoa huduma ya Jukwaa la Usambazaji (“Mmiliki Duka”); matumizi yako ya Programu ni lazima yaambatane na Sheria za Huduma za wakati huo za Jukwaa la Usambazaji la Mmiliki Duka; Mmiliki Duka ni mtoaji tu wa huduma ya wa Jukwaa la Usambazaji ambako ulipakua Programu;

Ni sisi pekee, na si Mmiliki Duka, tunawajibikia Programu;

Mmmiliki Duka hana jukumu wala dhima kwako kuhusiana na Programu au Sheria hizi; na

unatambua na kukubali kwamba Mmiliki Duka ni mnufaika mwingine wa Sheria inavyohusiana na Programu.

16.9 Apple App Store. Sehemu hii inatumika ambapo Programu zimepakuliwa kutoka kwenye Apple App Store. Unatambua na kukubali kwamba Sheria ni kati yako na sisi, si Apple, Inc. ("Apple") na kwamba Apple haina wajibu wowote kuhusiana na Programu au maudhui yaliyo ndani yake. Matumizi yako ya Programu ni lazima yaambatane na Sheria za Huduma za App Store.

Unatambua kwamba Apple haina jukumu lolote lile la kutoa huduma zozote za udumishaji na usaidizi kuhusiana na Programu. Endapo kuna wakati wowote ambapo Programu inakosa kuambatana na waranti zozote husika, unaweza kuarifu Apple, na (inapofaa) Apple itakurejeshea fedha ulizotumia kununua Programu; kwa kiwango cha juu zaidi kinachoruhusiwa na sheria husika, Apple haitakuwa na jukumu lingine lolote la waranti kuhusiana na Programu, na madai, hasara, dhima, uharibifu, gharama zingine zozote zinazohusiswa na ukosefu wowote wa kukosa kuambatana na waranti yoyote zitatawaliwa na Sheria hii na sheria yoyote husika kwetu kama mtoaji Programu.

Unatambua kwamba Apple haina wajibu wa kushughulikia madai yoyote yako au mhusika yeyote mwingine kuhusiana na Programu au umiliki wako na/au matumizi yako ya Programu, ikijumuisha, lakini sio tu: (i) madai ya shima ya bidhaa; (ii) dai lolote kwamba Programu zinakosa kuambatana na hitaji lolote husika la kisheria au kikanuni; na (iii) madai yanayoibuka chini ya ulinzi wa mtumiaji au sheria sawa; na madai yote kama hayo yanatawaliwa tu na Sheria hizi na sheria yoyote husika kwetu kama mtoaji Programu.

Unatambua kwamba, endapo kutakuwa na dai lolote la mhusika mwingine kwamba Programu au umiliki au matumizi yako ya Programu yanakiuka haki za mali bunifu za mhusika huyo mwingine, ni TFH, si Apple, itawajibika kuhakikisha uchunguzi, ulinzi, fidia na utekelezaji wa dai lolote kama hilo la ukiukaji haki za mali bunifu kwa kiwango kinachohitajika na Sheria.

Unawakilisha na kutoa hakikisho kwamba (i) haupo katika nchi ambayo ipo chini ya marufuku ya Serikali ya Marekani, au ambayo imetajwa na Serikali ya Marekani kuwa nchi "inayosaidia ugaidi"; na (ii) haujaorodheshwa kwenye orodha yoyote ya Serikali ya Marekani ya watu waliopigwa marufuku au wanaozuiliwa.

Wewe na TFH mnatambua na kukubali kwamba Apple, na kampuni tanzu za Apple, ni wanufaika wengine wa Sheria za Huduma kuhusiana na leseni yako ya Programu, na kwamba, baada ya wewe kukubali sheria na masharti ya Sheria za Huduma, Apple itakuwa na haki (na inaonekana kuwa imekubali kuwa ina haki) ya kutekeleza Sheria za Huduma kama inavyohusiana na leseni yako ya Programu dhidi yako kama mnufaika mwingine hapa.

TFHUSERTOS20241017 - AT